Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimuaga Sheha wa Shehia ya Tomondo Mohd Omar Said { Kidevu } anayekwenda Nchini India kwa Uchunguzi na Matibabu zaidi baada ya kumwagiwa Tindi kali usiku wa Tarehe 22 Mei 2013.
Sheha
Kidevu alikuwa akipatiwa huduma ya matibabu katika Hospitali Kuu ya
Rufaa Mnazi Mmoja kwa takriban Mwezi mmoja baada ya tukio hilo.Sheha wa Shehia ya Tomondo Moha Omar Said Kidevu akitoa shukrani kwa SMZ kwa kufanikisha safari yake ya kwenda matibabuni Nchini
India mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ambae
hayupo pichani wakati alipokwenda kumuuga rasmi kwa safari hiyo.Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
************************************
Sheha
wa Shehia ya Tomondo Wilaya ya Magharibi Bwana Mohd Omar Said { Maarufu
Kidevu } ameondoka Zanzibar kuelekea Nchini India kwa ajili ya Uchunguz
na matibabu zaidi baada ya kumwagiwa Tindi kali { Acid } na mtu
asiyejuilikana Usiku wa tarehe 22 Mei Mwaka huu wa 2013.
Sheha
Mohd Kidevu alikuwa akipatiwa huduma zamatibabu katika Hospitali Kuu ya
Mnazi Mmoja kwa takriban Mwezi Mmoja sasa kutokana na kuathirika sehemu
ya kulia ya kifua chake, Bega pamoja na baadhi ya maeneo ya mapaja.
Mgonjwa
huyo ameondoka na Ndege ya shirika la ndege la Oman kwa kupitia Muscut
na amewasili Mjini Chenai Nchini India mapema leo tarehe 21/6/2013 saa
12.30 za asubuhi akiambatana na Daktari wake.
Akimuaga
sheha huyo hapo katika wadi yake ya Mapinduzi Kongwe Mnazi Mmoja Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alimuombea sheha Mohd
Kidevu safari ya mafanikio itakayomletea hafaja njema.
Bwana
Mohd Kidevu alisema Mtu huyo alianza kutimua mbio baada ya kufanikiwa
kufanya dhambi hiyo kitendo ambacho akalazimika kuomba msaada kwa
wasamaria wema lakini hatimae ilishindikana kutokana na kuzidiwa kwa
maumivu makali yenye kuchoma kama moto.
Sheha
huyo wa Shehia yaTomondo aliendelea kumfahamisha Balozi Seif kwamba
hali yake hivi sasa inaendelea vyema na ameshaanza
kupatamatumainikufuatiajicho lake
kuanzakuonaingawabadoanakabiliwanamaumivukatikasehemuyakeyausoni.
Naye
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alimuomba Sheha huyo wa
Tomondo kuwa na moyo wa subra wakati wa kipindi hichi kigumu cha huduma
za matibabu.
Balozi
Seif alimuhakikishia Bwana Mohd Kidevu kwamba Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar itaendelea kufuatilia matibabu ya afya yake hadi atakapopata
nafuu na kurejea nyumbani kuendelea na harakati zake za kimaisha kama
kawaida.
Naye
sheha wa shehia ya Tomondo Mohd Omar Said { Kidevu } aliishukuru
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada zake zilizosaidia
kufanikisha kwa safari yake ambayo imempa faraja kubwa.
Sheha
Kidevu alisema maumivu yaliyokuwa yakimkabili ndani ya wiki hii hasa
wakati wa kula imepunguwa kidogo kufuatia huduma za karibu alizokuwa
akipatiwa na madaktari wanaomuhudumia.
Akizungumza
na vyombo vya Habari nje ya Wodi ya Mapinduzi Kongwe hivi karibuni
wakati alipomkagua sheha huyo kwa mara ya kwanza Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali Kuu imesikitishwa na
vitendo hivyo viovu vinavyoleta athari kwa Binaadamu.
Balozi
Seif alisema tabia hiyo mbaya inayoonekana kuanza kuchipua hapa Nchini
ikibeba ufinyu wa imani inaanza kuleta hofu miongoni mwa wananchi katika
kuendelea na harakati zao za kimaisha za kila siku.
Alisema
Serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi itaendelea na uchunguzi wa
kufuatilia matukio hayo na kamwe haitasita kuwachukulia hatua za
kisheria kwa kuwafikisha katika mkondo wa sheria wale wote
watakaobainika kuhusika katika vitendo hivyo.
Hili ni tukio la tatu kuwahi kutokea la kumwagiwa watu tindili kali ndan
ya mkoa wa mjini Magharibi likiwahusisha aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa
Baraza la Manispaa Ndugu Rashid Ali Juma pamoja na Katibu wa Fufti Mkuu
wa Zanzibar Sheikh Fadhil Suleiman Soraga.
Othman KhamisAme
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
23/5/20
Post a Comment