Aliyekuwa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Kilolo Marehemu Mohamed Ngwalima,
alipotembelea mto Ruaha mkuu eneo la Nyanzwa ambalo maji ya mto huo
yamekauka.
-------------------------------------------
KATIKA hali isiyo
ya kawaida, mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa, Mohamed
Ngwalima amekutwa amekufa akiwa katika Kochi la nyumbani kwake, baada ya kutoka
safarini, kifo ambacho kimeibua maswali mbalimbali kwa wananchi juu ya kifo
hicho cha ghafla.
Akizungumzia kifo
hicho cha ghafla mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Joseph Muhumba
alisema alishangazwa na taarifa ya kifo hicho kwani muda mfupi walikuwa
wameachana na marehemu, kwani walikuwa wote jijini Dar es salaam ambako walikuwa
katika kikao cha wadau wa zao la Chai.
“Tulikuwa wote
Dar es salaam ambako tulikwenda kufuatilia masuala ya kiwanda chetu cha Chai,
Mkurugenzi wangu Mohamed Ngwalima alikuwa ni mzima, tulikuwa wote kwenye kikao
na watu wa Chai, nimeachana nae mie nikielekea Dodoma, lakini jana alikuwa
ameanza safari ya kuja Kilolo, na asubuhi tumewasiliana naye akasema yupo
Kibaha, lakini nikashangaa ninapewa taarifa kuwa amekufa ghafla, kwani sikupata
maelezo yoyote ya awali kuwa ameumwa nini, kwa kweli tukio hili limetushitua
sana sisi kama madiwani, watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo na
wananchi wote kwa sababu limekuwa nila ghafla sana,” Alisema
Muhumba.
Alisema taarifa
aliyopokea ilisema marehemu alifariki akiwa amekaa katika Kiti (Kochi) la sebule
ya nyumbani kwake, muda mfupi baada ya kufika akitokea safarini Dar es salaamu,
ambako alikwenda kufuatilia masuala ya mpango wa wa kiwanda cha
chai.
Muhumba alisema
siku moja wakiwa katika ziara ya kikazi jijini Mwanza marehemu alimueleza kuwa
anatatizo la ugonjwa wa Kisukari, lakini tangu kuanza kazi katika wilaya hiyo
hajawahi kuugua, kwani alikuwa akijituma sana katika shughuli za
maendeleo.
Aidha alisema
Marehemu hakuwahi kutoa taarifa za kuumwa, na kuwa kifo chake ni pigo kwa Wilaya
ya Kilolo na Taifa zima na watamkumbuka kwa utendaji wake wa kazi kupitia
maamuzi mbalimbali ya vikao, huku akiwa mfuatiliaji wa masuala ya
kiuchumi.
Naye Benson
Kilangi ofisa kilimo, mifugo na ushirika Wilaya ya Kilolo ambaye ni mratibu wa
shughuli za mazishi alisema marehemu aliingia katika Wilaya ya Kilolo majira ya
saa kumi na moja jioni akitokea safarini Dar es salaam ambapo hakuwa na dalili
zozote za ugonjwa wala kuumwa.
Kilangi alisema
muda mfupi baada ya kuachana na mkurugenzi huyo alipigiwa simu na mke wa
marehemu akimueleza kuwa Ngwalima amezidiwa na baada ya kufika nyumbani hapo kwa
marehemu walikuta tayari mkurugenzi huyo akiwa
ameshafariki.
“Mkurugenzi
aliingia hapa Kilolo majira ya saa kumi na moja jioni akitokea Dar es salaam, na
alipofika alimwambia dereva ampeleke nyumbani na huko kwa mujibu wa maelezo ya
mke wake marehemu alisema alifika na kukaa kwenye Kochi ambapo ndipo mahali
alipofia, lakini mimi ni mtu wake wa jirani sana nilipoonana naye alikuwa na
hali njema kabisa, kwani kama angekuwa alikuwa anaumwa ningemtambua na
tungechukua jukumu la kumpeleka Hospitali kupata matibabu,” Alisema
Kilangi.
Aidha alisema
marehemu hakuweza kupatiwa matibabu yoyote, kwani hata walipomuita daktari
walipata taarifa ya kuwa tayari mkurugenzi huyo alikuwa
amekufa.
Alisema muda wa
taarifa na kitendo cha kufika nyumbani hapo kwa marehemu haikumchukua muda mrefu
kwani nyumba yake ipo jirani sana na jengo la Halmashauri ya Wilaya hiyo, na
kuwa hatua ya kifo hicho cha ghafla ni pigo kubwa kwao na wananchi wa Wilaya
hiyo.
Kilangi alisema
mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali yam Koa wa
Iringa, na wanafanya mpango wa kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Ikwiriri
Rufiji kwa ajili ya mazishi.
Marehemu Mohamed
Ngalima alizaliwa mwaka 57 katika kijiji cha Ikwiriri Rufiji, na alikuwa na
elimu ya shahada ya Uchumi ambapo alifanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya
Mtwara kama mchumi wa Wilaya hiyo, na mwaka 2007 aliteuliwa kuwa mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani
Arusha.
Na mwaka 2012
alihamishiwa Wilaya ya Mtwara ambapo mwaka 2013 alipelekwa katika Halmashauri
ya Wilaya ya kilolo mkoani Iringa hadi unapomfika umauti siku ya tarehe 25
mwezi sita 2013 saa moja kamili jioni, katika nyumba yake aliyokuwa akiishi na
familia yake.
Na mwili wa
marehemu unataraji kuzikwa kesho tarehe 27 mwezi june kwani taratimu za msafari
zimeanza katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa, ambako mwili wa marehemu upo
(Mortuary) huku watumishi mbalimbali wa serikali na sekta binafsi pamoja na
wananchi mkoani Iringa wakiwa eneo hilo kwa ajili ya kutoa heshima zao za mwisho
na kuuaga mwili wa marehemu ili kuanza safari ya kuelekea Rufiji katika makao ya
milele.
BWANA ALITOA,
BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA HIHIMIDIWE.
AMINA.
Post a Comment