Mheshimiwa Lema akiwahutubia wananchi kabla ya
tukio kutokea (Picha na Seria wa Arusha 255)
Mwenyekiti wa Chadema, Mh Freeman Mbowe akiwasili
viwanja vya Soweto, Kata ya Kaloleni Jijini Arusha jioni ya leo katika Mkutano
wa Chadema kufunga kampeni zake.
******
Mlipuko wa kishindo ulisikika katika viwanja vya Soweto mjini Arusha, ikiwa ni takribani saa 12 jioni, wakati mheshimiwa Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA wakiwa katika harakati za kufunga kampeni za uchaguzi wa madiwani unaotarajiwa kufanyika hapo kesho.
Tukio kama hili lilitokea takribani mwezi mmoja uliopita jijini Arusha lakini kabla uchunguzi ukiwa bado haujatoka, mengine yameibuka upya!!!!!!!
Ripoti kamili haijatoka kutoka jeshi la polisi, lakini inahofiwa kuwa watu wanne wamepoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa. Please pray for us!!!
Uwanja wa Soweto ambapo Mkutano wa Chadema kufunga kampeni za kuwania Udiwani Kata ya Kaloleni Jijini Arusha ulikuwa unafanyika umegeuka kuwa uwanja wa vilio baada ya kinachodhaniwa kuwa bomu kulipuka na kuua watu watatu na zaidi ya 50 kujeruhiwa vibaya huku baadhi yao wakiwa wamevunjika miguu.
Katika Mkutano huo walikuwapo pia Mwenyekiti wa Chadema naa Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema sambamba na viongozi wengine wa Chadema Mkoa wa Arusha lakini bahati nzuri Mbowe na Lema ambao walokuwa vinara katika Mkutano huo hawakudhurika moja kwa moja na mlipuko huo.
Mlipuko huo ulitokea mbele ya gari ambalo lilikuwa ni jukwaa la matangazo mara baada tu ya Mh Mbowe, Lema na viongozi wote waliokuwa jukwaa kuu kushuka chini na kujichanganya katikati ya watu wakikusanya michango ya watu, hali inayoashiria mrushaji huenda lilenga kuwajeruhi viongozi hao.
Miili ya marehemu na majeruhi walipelekwa hospitali ya Mt Meru lakini hawakupokelewa baada ya kilichoelezwa ni vurumai iliiyoletwa na mamia ya wafuasi wa Chadema waliokuwa na hasira baada ya wenzao kuuawa.
Hali ikiwa bado tete viwanjani hapo, magari kadhaa ya askari polisi yalifika huku askari wakiwa na silaha lakini walilazimika kupiga mabomu ya machozi kadhaa hewani na kisha kuondoka kutokana na baadhi ya wananchi waliokuwa na hasira kuwafuata na kupaza sauti wakitaka wawaue pia.

Kijana mmoja muuza machungwa aliieleza blogu hii kuwa aliyerusha bomu hilo alitokea upande wa nyuma ya jukwaa kuu na badae kukimbilia nyumba zilizojirani.
CREDITS: LIBENEKE/NOISE OF SILENCE BLOG, SERIA WA ARUSHA 255, MPEKUZI , DJ SEKI, NA ASILI BLOGS
Post a Comment