Mwanamke
mkulima mkazi wa kijiji cha Kisana wilaya ya Iramba mkoa wa Singida
Sayuni Ramadhani (42), amehukumiwa adhabu ya kutumikia jela miaka mitatu
baada ya kukiri kosa la kumng’ata uume mume wake na kubakia ngozi ndogo
ukatike.
Mwanaume aliyeng’atwa uume wake na mke wake ni Onesmo Nathania (42).
Mapema
mwendesha mashitaka mkaguzi wa polisi Vicent Ndasa, alidai mbele ya
hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Iramba Mrisho Mrisho, kuwa
mnamo Juni 4 mwaka huu saa 12.00 jioni huko katika kijiji cha kIsana,
mshitakiwa kwa makusudi aling’ata kwa nguvu uume wa mume wake Onesmo na
kumsababishia maumivu makali.
Ndasa
amesema siku ya tukio, wanandoa hao waliporejea nyumbani kutoka kwenye
klabu ya pombe za kienyeji mali ya kijiji cha Kisana, kulitokea
kutokuelewana na kupelekea waanze kugombana.
Amesema
wakati wanaendelea kupigana, Onesmo alizidiwa nguvu na aliangushwa
chini kisha kugandamizwa na zipu yake ya suruali iliweza kufunguliwa.
Baada
ya zipu ya suruali ya Onesmo kufunguliwa, mshitakiwa alifanikiwa kuutoa
uume wa mume wake kutoka ndani ya nguo ya ndani na kuutia mdomoni na
kuung’ata kwa nguvu na nusura aukate vipande viwili.
Mwendesha
mashitaka huyo, amesema kuwa mlalamikaji Onesmo alipiga yowe na
majirani wema walifika mara moja na kumkimbiza katika zahanati ya kijiji
kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Kabla
ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Ndasa aliiomba mahakama hiyo kumpa adhabu
kali mshitakiwa ili kuwa fundisho kwake na pia kuogofya wanawake
wanaotarajia kuwafanyia unyama wa aina hii ya kung’ata sehemu nyeti za
waume zao.
Kwa
upande wake mshitakiwa Sayuni aliiomba mahakama hiyo imwonee huruma na
kumpa adhabu nafuu kwa madai kuwa hilo ni kosa lake la kwanza toka
amezaliwa na vile vile ana jukumu kubwa la kushirikiana na mume wake
kulea idadi kubwa ya watoto walionao.
Akisoma
hukumu hiyo, hakimu mfawidhi Mrisho, alisema mahakama yake imezingatia
kwa makini maombolezo ya mshitakiwa na kufikia uamuzi wa kutoa adhabu ya
kutumikia jela miaka mitatu.
Post a Comment