Jeshi la
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeendelea na operesheni
mbalimbali kwa mafanikio, ikiwemo kukama wahalifu, kuokoa mali
zilzoibiwa na kuwadhibiti madereva wanaokiuka sheria za barabara.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam Suleiman Kova (pichani)
amesema jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata majambazi wanane hatari
wanaojihusisha na uporaji wa mali za raia wa kigeni ufukweni mwa bahari
ya Hindi (Coco Beach).
Pia Kamanda
Kova amesema Jeshi hilo limemkamata mtunza bustani aitwaye Philemon
Laiza mwenye umri wa miaka 27 mkazi wa Mikocheni B maeneo ya nyumba za
serikali anayefanya kazi nyumbani kwa Jaji Kileo, akituhumiwa kuhusika
na mauaji ya Perpetua mainab (30) mtumishi wa ndani raia wa Kenya
aliyekutwa amekufa baada ya mwili wake kuchinjwa sehemu ya shingo,
jeraha mkono wa kushoto karibu na kiganja na jeraha kwenye paji la uso.
Katika
tukio lingine, Jeshi hilo limefanikisha kuokolewa kwa mali ya Wachina
(Power Tiller) zenye thamani ya Tsh. 157,000,000/= ikiwa ni pamoja na
kumkamata tapeli hatari Satara Emmanuel (42) aliyeitapeli kampuni ya
AFRICATIC iliyopo Nyerere Road kwa kuonyesha nyaraka za kugushi kwamba
ameshinda zabuni ya ununuzi wa Power Tiller katika Halmashauri ya Mbulu
hali akijua anadanganya.
Kamanda
Kova amesema Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm limemfukuza kazi askari
polisi wa kike aitwaye WP AMISA ambaye alikuwa akifanya kazi katika
kituo cha Polisi Magomeni baada ya kumtia hatiani kwa utovu wa nidhamu
na kukiuka maadili ya Jeshi la Polisi.
Aidha
katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Kanda Maalum kupitia kitengo cha
usalama barabarani limeendelea na msako mkali juu ya madereva wanaokiuka
sheria za usalama barabarani ambapo jumla ya makosa 2,148 yamekamatwa.
Idadi magari binafsi 636 yamekamatwa, daladala 1001, pikipiki 315 na magari ya mizigo kupakia abiria 59, ambapo fedha za faini zilizokusanywa ni Tsh. 64,440,000/= na madereva waliofikishwa mahakamani ni watani (5).
Post a Comment