Mkuu
wa Kitengo cha Vipaji na Uendelezaji wa Biashara wa Kampuni ya Rockstar
4000 Bi. Christine Mosha “Seven” akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo ambapo amesema amefurahishwa sana kufanya kazi
na Orijino Komedi ambao ni watu wenye vipaji vya hali ya juu na kuingia
mkataba na Kampuni ya Nexus Consulting Agency ambapo kwa pamoja
wamedhamiria kukuza na kubadilisha dhama ya vipaji na sanaa kutoka ilipo
na kuwa ya kimataifa. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Nexus Agency Bw.
Bobby Bharwani na kulia ni Muandaaji wa vipindi vya Orijino Komedi
Sekioni David.
Mkurugenzi
Mkuu wa Nexus Consulting Agency Bw. Bobby Bharwani (kushoto) akieleza
kuwa kwa upande wa kampuni yao kushirikiana na Orijino Komedi ni kitu
muhimu kwa Nexus kwani siku zote imekuwa ikitamani kufanya kazi kwa
karibu na kundi hilo na kuthamini kazi zao kutokana na vipaji vya hali
ya juu walivyokuwa wakionyesha wasanii wa kundi hilo.
Picha
ya pamoja kati viongozi wa makampuni ya ‘Nexus Consulting Agency’ na
‘Rockstar 4000′ na wasanii wa kundi la Orijino Komedi mara baada ya
kutolewa kwa taarifa ya kundi hilo kuingia mkataba na makampuni hayo.
Na. Mo Blog Team.
Kundi
la kipaji cha Televisioni “Orijino Komedi” linaloongoza nchini kwa
vipindi vyake kupitia televisionilimeingia mkataba na Kampuni ya Nexus
Consulting Agency kwa kushirikiana na Rockstar 4000, ambao utakuwa ni
mkataba wa kwanza kwa wasanii wa luninga kupitia kampuni ya Nexus.
Nexus
imenunua haki zote za usimamizi wa biashara na uongozi wa kundi hilo
ambalo linajulikana sana nchini kupitia vichekesho vyake vinavyoonyeshwa
na vituo vya television na matamasha mbalimbali, ambapo mkataba huo
utakuwa ni kwa ajili ya kusimamia kipindi hicho cha vichekesho
kinachoundwa na wachekeshaji saba ambao ni Joti, Macreagan, Masanja,
Wakuvanga, Mpoki, Vengu na Seki David ambacho kimekuwa hewani kwa
mfululizo wa miaka sita.
Kwa
kushirikiana na Rockstar 4000, Nexus imesema itahakikisha inaendeleza
vipaji vya wasanii wa kundi hilo ili vipaji vyao viweze kufikia kiwango
cha juu cha ufanisi ndani ya Afrika na Kimataifa kwa ujumla.
Post a Comment