Na Mwandishi Wetu
TAMASHA la Mastaa Chipukizi lililokuwa lifanyike Jumamosi
Juni 29 kijiji cha wasanii Mwanzega Mkuranga limeahirishwa ili kutoa nafasi
kwa wasanii na viongozi mbalimbali
kushiriki kikamilifu katika maandalizi na mapokezi ya Rais wa Marekani, Baraka Obama.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Caaasim
Taalib alisema jana kuwa wanachama wengi waliokuwa washiriki tamasha hilo
watakuwa katika maandalizi ya ujio wa Rais Obama hivyo litafanyika mwezi Agosti
baada ya sikukuu ya Idd el Fitri.
Taalib alisema anawaomba radhi wananchi wa Mkuranga,
viongozi mbalimbali na wasanii washiriki wa tamasha hilo waliokuwa wamejiandaa
kuonesha vipaji vyao katika tamasha hilo .
‘Tumeamua kutoa nafasi hii kwa wanachama wa SHIWATA ili
washiriki kikamilifu kudumisha amani katika wakati huu ambao tunatembelewa na
Rais Obama na wasanii washiriki kikamilifu, tunaomba tutoe taarifa katika
vyombo vya dola mara tunapoona kuna unjifu wa amani’ alisema Taalib.
Mwenyekiti huyo alisema mgeni rasmi aliyekuwa ameandaliwa,
Naibu Waziri wa Kilimo, Adam Malima amepelekewa ujumbe huo pamoja na Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wabunge wa Dar es Salaam
nao wamearifiwa kuhusu kusogezwa mbele tamasha hilo .
Alisema sambamba na tamasha hilo, SHIWATA ilikuwa ikabidhi
nyumba kwa mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’,
Jellah Mtagwa na wasanii wengine 14 ambao wamekamilisha michango ya ujenzi wa nyumba zao katika kijiji chao cha Mwanzega
Kimbili, Mkuranga.
Wengine watakaokabidhiwa nyumba zao ni msanii maarufu
nchini, Lumole Matovola ‘Big’ wa Bongo movie ambaye ni wanachama wa SHIWATA
wangine ni Mwandishi wa Habari, Josephine Moshi, Farida Ndimbo wa Jeshi la
Magereza, Flora Kafwembe wa JKT Mgulani na Nyanza Kisadugwa wa Jeshi la Ulinzi
la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Mpaka sasa SHIWATA
imejenga nyumba 24 kwa ajili ya wasanii katika eneo la hekari 300 na
wanajiandaa kulima shamba la hekari 500 walizonazo ili kujikwamua kimaish
Post a Comment