DODOMA.
Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kimemalizika mjini Dodoma huku kukiwa na taarifa kuwa chama hicho kimeweka msimamo wa kutaka kuwepo kwa mfumo wa Serikali mbili katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kimemalizika mjini Dodoma huku kukiwa na taarifa kuwa chama hicho kimeweka msimamo wa kutaka kuwepo kwa mfumo wa Serikali mbili katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mchakato wa Katiba Mpya ya Tanzania upo katika
hatua ya rasimu na watu mbalimbali kupitia Mabaraza ya Katiba, wamekuwa
wakitoa maoni yao.
Tayari Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete
ametangaza kuwa chama hicho kitakuwa moja ya mabaraza ya katiba na
kupata nafasi ya kuichambua, kuijadili na kutoa maoni kuhusu rasimu
ilitolewa hivi karibuni na Tume ya Mabad
iliko ya Katiba chini ya mwenyekiti wake Jaji mstaafu Joseph Warioba.
iliko ya Katiba chini ya mwenyekiti wake Jaji mstaafu Joseph Warioba.
Habari za ndani zilisema kuwa kikao hicho
kilichoongozwa na Rais Kikwete kilijadili mchakato wa Katiba Mpya,
masuala ya maadili ndani ya chama na kuyatolea uamuzi.
Hata hivyo mmoja wa watendaji ndani ya chama hicho
alisema kikao kilikuwa cha kawaida na kwamba kilikuwa kinapitia
majukumu na kwamba hakuna kubwa lililojadiliwa. Habari zaidi zinadai
kuwa mbali ya kuunga mkono mfumo wa Serikali mbili, CCM imetoa adhabu
kwa wanachama wake wawili ambazo zitatangazwa katika siku iliyopangwa.
Mmoja wa watoa habari alilieleza gazeti hili kuwa
uamuzi uliotolewa na kamati hiyo, utawasilishwa kwa wanachama wake kwa
utaratibu uliopangwa na kwamba wabunge wa CCM wataelezwa katika kikao
chao kitakachofanyika keshokutwa Jumamosi katika Ukumbi wa Pius Msekwa
mjini Dodoma.
“Sisi wabunge tunategemea kuelezwa uamuzi wa CC
katika kikao chetu cha Jumamosi, tumeambiwa kikao hicho ni muhimu na
tuhudhurie bila kukosa,” kilieleza chanzo hicho jana jioni.
Habari zaidi zilisema wakuu wote wa mikoa na
wilaya tayari wapo mjini Dodoma na kwamba watakutana na Waziri Mkuu
katika mkutano wa kichama uliopangwa kufanyika jana usiku.
Zinapasha kuwa katika mkutano huo uliotarajiwa
kufanyika katika Hoteli ya Dodoma, MaRC na MaDc hao wataelezwa mkakati
na msimamo wa chama hicho kuhusu mchakato wa Katiba Mpya.
CHANZO MWANANCHI.
CHANZO MWANANCHI.
Post a Comment