|
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA RUNGWE AKIONGEA NA BARAZA LA
MADIWANI NA WATENDAJI KATIKA KIKAO MAALUM CHA KUUUGAWA MKOA WA MBEYA KUWA MIKOA
MIWILI |
|
MWENYEKITI WA KIKAO MAALUM CHA BARAZA LA MADIWANI RUNGWE
ALFRED MWAKIPIKI AKATOA TAMKO KUWA MAKAO MAKUU YA MKOA MPYA UWE TUKUYU, NA
MAPENDEKEZO YA WILAYA YAKIWA NI 1. RUNGWE 2. ILEJE 3. KYELA 4. BUSOKELO
ITAMBULIKE KAMA WILAYA ILI KUUNDA MKOA WENYE WILAYA
NNE |
|
DAS ALINANUSWE MWALUFUNDA AKITOA TAARIFA YA SERIKALI
BAADA YA MCHAKATO HUU KUANZA ILI KUGAWA MKOA WA MBEYA NA KUWA MIKOA
MIWILI
|
|
Afisa utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ndugu
Mbai akisoma mapendekezo ya wilaya ya Rungwe kwa madiwani wa Halmashauri ya
wilya ya Rungwe kwa ajili ya kuugawa mkoa wa Mbeya.
|
|
Mmoja wa madiwani ndani ya baraza hilo ndugu Anyimile
Mwasakilali Kata ya Kawetere( NCCR) kupinga vikali suala la ugwaji wa mkoa mbeya
kutokana na kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazo ikabili wilaya hiyo ya
Rungwe |
|
Diwani wa kata ya Bagamoyo katika Halmashauri ya Wilaya
ya Rungwe. Bashiru Madodi akichangia hoja ya kuugawa mkoa wa Mbeya
|
|
JENGO LA OFISI YA HALMASAHURI YA
RUNGWE
Kitendo cha serikali kusogeza madaraka kwa karibu zaidi
na wananchi ili kuwawezesha kuamua mambo yanayo husu maisha maendeleo ya kila
siku imechangia kwa asilimia kubwa baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya
Runwe kuamua kutumia hoja hiyo kuugawa mkoa mbeya na kuwa mikoa
miwili.
Moja ya sababu ambazo zimepelekea baraza hilo kutumia
hoja hiyo kama kigezo mojawapo cha kujipatia mkoa mpya ni pamoja na kupanga
kubuni na kutekeleza kulinda na kuendesha mipango yao kwa kutekelezwa kitaalamu
zaidi katika kuwaletea maendeleo wananchi endapo mkoa huo
utapatikana.
Hatua hiyo imefikiwa katika kikao maalumu cha baraza la
madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kilicho keti kujadili mpango wa
ugawaji wa Mkoa wa mbeya kuwa mikoa miwili ambapo katika katika kikao hicho
baraza hilo la madiwani limefikia maamuzi ya kuugawa mkoa huo wa mbeya na
kuuita mkoa wa Rungwe ambapo makao makuu yake yamependekezwa kuwa Mamlaka ya mji
mdogo Tukuyu.
Akiwasilisha mapendekezo ya kamati tendaji( CMT) na
kamati ya fedha Ndugu Noel Mahyenga amesema wanaipongeza serikali ya awamu hii
kwa hatua yake ya kukubali kutoa mapendekezo yake ya ugwaji wa mkoa wa mbeya kwa
lengo la kupunguza mzigo na majukumu Ya serikali kwa lengo la kuwaletea
maendeleo wananchi.
Amesema katika kufanya hayo serikali imekuwa ikigawa
mikoa wilaya na Halmashauri ili kurahisisha utawala na uendeshaji wa taasisi
hizo katika hatua moja wapo ya utekelezaji wa malengo yake
yaliyokusudiwa.
Wamesema kulingana na ukubwa wa eneo na idadi
ya watu katika mkoa huo wa mbeya imekuwa vigumu kwa watumishiwaliopo
sekretalieti ya mkoa kusimamia kikamilifu maendeleo ya mkoa kwa maana ya kutoa
ushauri wa kitaalamu pamoja na kusimamia utekelezaji wa shughuli mablimbali za
kimaendeleo kwa wakati muafaka ili kukidhi haja inayokuwepo wakati inapo
hitajika.
Hata hivyo baraza hilo kwa nguvu moja limekubali kutoa
moja ya majengo yake mapya yaliyojengwa ndani ya halimashauri hiyo kuwa ofisi ya
mkoa ambapo ujenzi huo umetumia fedha za ndani pamoja na baraza hilo pia
limependekeza halmashauri ya wilaya ya busokelo iwe wilaya ili kufanya mkoa kuwa
na wilaya nne ambazo ni Kyela,Ileje na Busokelo badala ya wilya tatu zilizopo
hivi sasa.
Pamoja na baraza zima la halmashauri hiyo kupitisha hoja
hiyo ya ugawaji wa mkoa mmoja wa madiwani ndani ya baraza hilo ndugu Anyimile
Mwasakilali Kata ya Kawetere( NCCR) kupinga vikali suala la ugwaji wa mkoa mbeya
kutokana na kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazo ikabili wilaya
hiyo.
Moja ya changamoto hizo ni pamoja na kata yake kuto
patiwa ofisi ya Afisa Mtendaji kwa muda mrefu sasa hivyo amehoji juu ya
kuanzishwa kwa mkoa mpaya wakati bado kuna changamoto nyingi hivyo kitendo cha
hatua hiyo kitawabebesha mzigo mkubwa wananchi wake pamoja na serikali kwa
ujumla. Mbeya yetu
|
on Thursday, June 20, 2013
Post a Comment