Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TANSEED KUDHIBITI MAGUGU HATARI YA KIDUHA




5114492939 e53840e319 cf8b1KAMPUNI ya mbegu ya TANSEED International yenye makao makuu mjini Morogoro imeandaa maonesho ya shamba darasa ya teknolojia mpya ya mbegu za mahindi ya TAN 222 kukomesha kiduha "trigaway maize"kwa ajili ya kudhibiti magugu hatari ya kiduha kwenye zao la mahindi.

Maonesho hayo yatafanyika kesho (Jumamosi) katika maadhimisho ya siku ya wakulima (Farmer Field Day) katika kijiji cha Mkuza wilayani Mheza ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa.
Ambapo yatahudhuriwa na watafiti wa mazao ya kilimo, wataalamu wa ugani, makampuni ya mbegu, wakulima, taasisi za serikali na zisizo za kiserikali mkoani humo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Isaka Mashuri leo jijini Dar es salaam katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari -MAELEZO alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya maadhimisho hayo yatakayofanyika mkoani Tanga.
Alisema lengo la maonesho hayo ni kuhamasisha wakulima, watafiti, washauri wa ugani, wasiasa, taasisi za serikali na zisizo za kiserikali pamoja na wadau wengine ni kuhusu tishio linatokana na magugu ya kiduha.
"Magugu ya kiduha yamekuwa ni tatizo kubwa kwa wakulima wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa kipindi cha miongo saba. Kiduha ni magugu tegemezi yanayojishikiza kwenye mizizi ya mazao ya nafaka na kunyonya maji , madini na virutubisho vingine." alisema Mashuri.
Mashuri aliongeza kuwa magugu hayo huharibu ya mahindi kwa kutoa sumu na kuweza kuangamiza mimea ya mazao hata kabla magugu hayajajitokeza juu ya ardhi.
"Magugu ya kiduha huzaa mbegu nyingi kati ya 5,000 hadi 200,000 kwa mmea mmoja, hivyo kufanya tatizo kuwa kubwa zaidi kwani mbegu za kuduha huweza kubaki zikiwa hai aridhini kwa muda mrefu zaidi ya miaka 20 na zaidi na kusababisha upungufu wa chakula kila mwaka, " alisema Mashuri.

Alisema kwamba inakadiriwa kuwa takribani hekari milioni 1.5 za ardhi Afrika Mashariki zimeathiriwa na magugu ya kiduha ambapo aliitaja mikoa iliyoathirika Tanzania na magugu hayo ni pamoja na Morogoro, Pwani , Tanga, Dodoma,Singida, Tabora, Shinyanga , Mwanza, Mara, Ruvuma, Iringa, Mbeya, Rukwa, Lindi na Mtwara na kubainisha kuwa ni zaidi ya ekari 1,500,000 zimeathirika.
Aidha Mashauri alieleza kuwa magugu hayo husababisha upotevu wa mavuno takribani tani milioni 1.7 za nafaka zenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 356 ambazo ni sawa na Sh.bilioni 584.6 za Kitanzania kwa mwaka.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la BASF Nchini Kenya linalojishughulisha na shughuli za madawa ya kilimo, Sammy Wairuingi alisema kuwa Tanzania tushangilie kwa furaha ya kuja kwa fursa hii ya teknolojia mpya kwani itasaidia kuzalisha chakula cha kutosha kulisha familia ,kufukuza njaa na umasikini.
Kampuni ya TANSEED inashirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mahindi na Ngano ' International Maize and Wheat Improvement Centre' (CIMMYT), Taasisi ya kimataifa ya 'African Agriculture Technology Foundation' (AATF) inayojishughulisha na kuunganisha sekta za umma na binafsi katika usambazaji wa teknolojia za kilimo, na kampuni ya madawa ya kilimo na majumbani BASF.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top