TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Yah:- Uchaguzi wa viongozi wa BFT.
Uchaguzi wa viongozi wa BFT uliopangwa Kufanyika tarehe
7/7/2013 jijini Mwanza, utafanyika kwa tarehe hiyo kama ulivyopangwa.
Kikao cha kamati ya utendaji ya BFT kilichofanyika juzi
katika ofisi za BFT kikiongozwa na Rais
wa shirikisho Joan Minja kimesisitiza kuwa uchaguzi utafanyika kama
ulivyopangwa na haujaairishwa kama baadhi ya kikundi cha watu wachache
wanaojiita wadau wanavyoweka pingamizi na
kupotosha kwa kuwashawishi
wajumbe wa mkutanao mkuu hasa kutoka mikoani kutohudhuria mkutano huo wa
uchaguzi,kwa manufaa yao binafsi na kinyume na katiba yetu.
Upotoshaji huo unafanywa na
Akaroly Godfrey aliyekuwa
kiongozi katika uongozi uliojiudhuru kutokana na kashfa za kusafirisha
madawa ya kulevya na kusababisha Tanzania kufutwa uanachama na chama cha ngumi
cha dunia (AIBA) na kusababisha
kutoshiriki mashindano,mikutano na shughuri zote za kimataifa za chama
cha ngumi cha Dunia AIBA. Naomba wadau na serikali kuwa makini na watu
wanaoshawishi kwa lengo la masilahi yao binafsi na kusababisha michezo kudolola
badala ya kusonga mbele.
Fomu za uchaguzi zilishaanza kutolewa na Baraza la Michezo
la Taifa (BMT) toka tarehe 4//2013 na zitaendelea kutolewa hadi tarehe 4/7/2013
jijini Mwanza na tarehe hiyo ndio
itakuwa siku ya mwisho ya kuchukua na kurudisha fomu, tarehe 5/7/2013 itatakuwa
siku ya usaili na utafanyika jijini mwanza, tarehe 6/7/2013 kupitia pingamizi
na kuzitolea maamuzi na tarehe 7/7/2013 ndio siku ya uchaguzi.
Kimsingi taratibu zote za kuitisha uchaguzi kwa mujibu wa
katiba yetu zimezingatiwa na zimekamilika.
Aidha BFT inatoa tamko kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu kufika
katika uchaguzi uchaguzi, ili kupata viongozi halali kwa mujibu wa katiba,
waendelee na shughuri za kuendeleza mchezo wa ndondi na kuaandaa timu ya taifa
kushiriki katika mashindano ya Afrika nchini Mauritius Sept. 2013.
BFT inatoa wito kwa watu wote wenye sifa, nia, moyo na uwezo
wa kuongoza wajitokeze kuchukua fomu za kugombea uongozi kwani wakati ndio
huu.
Makore Mashaga
Katibu Mkuu.
Post a Comment