Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu akimkabidhi Bi. Selina Otacho mshiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo vijana wahitimu wa vyuo vikuu kutoka maeneo mbalimbali mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 6 zilizotolewa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kutokana wazo lake la mradi wa utengenezaji wa sabuni za maji kushinda baada ya kupitiwa na wataalam wa Baraza la Uwezeshaji (NEEC) na Kituo cha Ujasiriamali cha Chuo Kikuu cha Dar es salaam jana.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu akiwaonesha washiriki wa mafunzo mafunzo ya kuwajengea Uwezo vijana wahitimu wa vyuo vikuu kutumia fursa zinazowazunguka kujiajiri wenyewe moja ya sabuni ya maji iliyowekwa katika vifungashio vya kisasa na kuahidi kuunga mkono juhudi zake za kupambana na umasikini.
Vijana waliohitimu mafunzo ya wiki 3 ya kujengewa uwezo wa kutumia fursa zinazowazunguka kujiajiri wenyewe na kuajiri wengine wakimsikiliza waziri wa Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu wakati akifunga mafunzo hayo.
Mshindi wa kwanza kati ya Vijana 40 walioshiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo vijana wahitimu wa vyuo vikuu Bw. Anthony Mhanda akionyesha kwa furaha mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 alizokabidhiwa na Baraza la Taifa la Uwezehaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) leo jijini Dar es salaam kufuatia mradi wa ufugaji wa nyuki aliouandika kushika nafasi ya kwanza.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya wiki tatu ya ujasiriamali Bw. Norvart Zedekiah leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Vijana nchini kutoka Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa miongoni mwa wataalam walioshiriki kuwajengea uwezo vijana hao. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu akiwa katika picha ya pamoja na vijana wahitimu wa vyuo vikuu kutoka mikoa mbalimbali nchini waliohitimu mafunzo ya wiki 3 ya kujengewa uwezo wa kutumia fursa zinazowazunguka kujiajiri na kuajiri vijana wengine leo jijini Dar es salaam.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Post a Comment