Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Wanafunzi Bora wazungumzia matokeo

SAID JUMA IRANDO2
*****
Mwanafunzi bora wa kwanza kitaifa katika matokeo yaliyorekebishwa ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka 2012, Said Irando kutoka Shule ya Sekondari Feza ya jijini Dar es Salaam, ameeleza kushangazwa na matokeo hayo kwa kuwa hakuyatarajia.
Mwanafunzi huyo ambaye tayari ameshaanza masomo ya Kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari Feza, alisema kuwa ingawa alisoma kwa bidii lakini hakudhani kama angeweza kushika nafasi ya kwanza kitaifa na kwamba anamini mafanikio yake kitaaluma yana ‘mkono wa Mungu’.
“Sikutegemea kabisa kuwa mwanafunzi bora, ingawa nilisoma kwa bidii kubwa nia yangu ilikuwa ni kutaka kufaulu tu; Ni Mungu amenisaidia,” alisema Irando.
Alisema kujituma katika masomo, mazingira mazuri ya kusomea na upatikanaji wa vifaa muhimu vya kujifunzia ndiyo yaliyomwezesha kusoma na kufanya vizuri.
Irando ambaye ni mtoto wa kwanza katika familia yenye watoto watatu, alisema kurekebishwa kwa matokeo ya kidato cha nne kulibadilisha alama za matokeo yake kutoka Daraja la kwanza akiwa na alama tisa hadi saba, zilizomfanya kuwa mwanafunzi bora kitaifa na mwafunzi bora wa kwanza kati ya wavulana kumi bora pia kitaifa.
Mwanafunzi huyo alibainisha kuwa pamoja na wazazi wake kuwa ni wafanyabiashara, yeye anatamani kuwa mhandisi ingawa bado hajajua atakuwa mhandisi katika tasnia gani.
“Natamani sana kuwa mhandisi hiyo ndiyo ndoto yangu ingawa bado sijajua nitakuwa mhandisi wa sekta gani,” alisema Irando.

Irando alisoma elimu ya msingi katika Shule ya Msingi J.K Nyerere ambako alifaulu na kuchaguliwa kujiunga na Sekondari Pugu, lakini wazazi wake waliamua kumpeleka Shule ya Sekondari Feza.
Naye mwanafunzi Joshua Azza kutoka Sekondari ya Wavulana Marian ambaye ameshika nafasi ya saba kitaifa kati ya wanafunzi kumi bora baada ya kupata daraja la kwanza akiwa na alama 11, alisema ameyapokea matokeo hayo kwa furaha akiamini atatimiza lengo lake la kuwa daktari wa upasuaji.
“Natarajia kuwa daktari wa upasuaji, kwa matokeo haya nadhani nitafanikiwa,” alisema Azza ambaye wazazi wake wote ni walimu alipozungumza na gazeti hili jana jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake Saidi Nchimbi kutoka Sekondari ya Feza, ambaye ameshika nafasi ya nane kati ya wanafunzi kumi bora kitaifa, alisema kuwa siku zote alikuwa akisoma kwa uwezo wake wote na kwamba alikuwa akitamani kufaulu kwenye mitihani yake yote aliyopewa.
Nchimbi amefanikiwa kushika nafasi hiyo baada ya kupata daraja la kwanza akiwa na alama nane. Katika matokeo ya awali mwanafunzi huyo alikuwa na alama 11.
MWANANCHI
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top