|
Jailo Rashid (30), Niza Hamis (24) na Medi Keya(33) ambao
kwa pamoja wanadhaniwa kumuua kwa maksudi, Ambrose Shayo(45) aliyekuwa ni
Mwenyekiti wa Umoja wa Saccos Taifa na Tazara Saccos ya Jijini
Mbeya. |
|
Hili ndilo eneo alilouwawa mwenyekiti huyo wa
saccos |
|
WATU watatu wamefikishwa mahakamani wakituhumiwa kutenda
kosa la kumuua kwa kukusudia aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha kuweka na Kukopa
(Saccoss), Mbeya
Akisoma mashtaka hayo, Mwendesha Mashtaka wa Serikali
Hebel Kihaka mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya Venance Mlingi
alidai Watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda kosa la mauaji kwa maksudi kinyume
cha Sheria ya Makosa ya Jinai kifungu cha 196 sura ya 16 kama ilivyofanyiwa
marekebisho mwaka 2002.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Jailo Rashid (30), Niza
Hamis (24) na Medi Keya(33) ambao kwa pamoja walimuua kwa maksudi, Ambrose
Shayo(45) aliyekuwa ni Mwenyekiti wa Umoja wa Saccos Taifa na Tazara Saccos ya
Jijini Mbeya.
Alisema watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo
April 20, Mwaka huu majira ya saa 3 usiku katika Kijiji cha Itagano Kawatere
Jijini Mbeya ambapo Marehemu alivamiwa na watu hao kisha
kumuua.
Kwa upande wake Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Venance
Mlingi alisema Kwa mujibu wa Sheria watuhumiwa hawaruhusiwi kujibu chochote
kutokana na Mahakama yake kutokuwa na uwezo wa kusikiliza Shauri la
Mauaji.
Aliongeza kuwa Shauri hilo limeletwa kwa ajili ya hatua
za awali ambapo baada ya upelelezi kukamilika litapelekwa Mahakama kuu kwa ajili
ya taratibu za kusikiliza, pia aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 3, Mwaka huu
itakapotajwa tena.
Na Mbeya yetu
|
on Thursday, June 20, 2013
Post a Comment