MAASKOFU
na Wachungaji wa Good News For All Ministry watoa sababu ya Timu ya
Taifa ‘Taifa Stars’ kukosa ushindi katika mechi yao naTimu ya Ivory
Coast iliyofanyika jumapili iliyopita Juni 16, mwaka huu.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo(jana) katika ukumbi wa mikutano wa Idara
ya Habari – MAELEZO jijini da res salaam, Askofu Charles Gadi amesema
kuwa kuna sababu nyingi zilizopelekea Taifa Stars kushindwa katika
mchezo wake na Ivory Coast ikiwa ni pamoja na matusi na mzaha unaofanywa
na wananchi wenyewe.
“Ndugu
waandishi, ni kweli goli la kwanza lilifungwa kwa maombi ya Watanzania
waliokuwa wakiomba, lakini matusi yaliyoendelea pale uwanjani ambayo
yanatukana maumbile ya mama, dada, wakwe na watoto zetu wa kike
yalitukwamisha.
“
Unapotukana kwa kutumia maumbile ya wakina mama ni sawa na
kuchafua,kujeli uumbaji wa Mungu kwa wakina mama. Hali hiyo hutuletea
laana ya kushindwa,” alisema Askofu Gadi.
Aliongeza
kuwa walianza kuiombea Taifa Stars toka mwaka 2012 ili ifanikiwe katika
mechi zake zote hivyo wana uchungu kwa kufungwa na timu hiyo ya kigeni.
Aidha
Askofu Gadi aliongeza kuwa pale uwanjani kulikuwa kumefurika watu wengi
hivyo kuhatarisha usalama wa watu walioko pale na hivyo ameiomba
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litoe tiketi kulingana na
idadi ya viti vilivyopo uwanjani.
Pia
Askofu Gadi amesema kuwa wana maombi ya siku elfu moja kwa ajili ya
kuliombea Taifa zima, mpaka sasa wamekaribia siku mia tano katika
maombi hayo hivyo wanaomba watu kutokwamisha maombi yao kwa kuacha
matusi.
“Naomba
Watanzania wamwogope Mungu kwa kuacha matusi na dhambi zao kwani
wakifanya hivyo nchi itakuwa na maendeleo na kuwa ya kistaarabu kwa
kuendeleza amani,” alisisitiza Mchungaji Leonard Kijuna.
Pia
Askofu Gadi ametoa wito kwa Serikali kuwa waweze kutunga sheria kuhusu
matusi kwamba endapo mtu atapatikana akitukana basi achukuliwe hatua
kama zilivyo nchi njingine,mtu akitupa bigijii anafungwa, kwani
itasaidia kutokomeza kabisa suala hilo.
Post a Comment