Jeshi la Polisi Mkoa Dodoma linawashikilia watu
wawili kwa tuhuma za kumvamia na kumshambulia Mheshimiwa MOSES S/O
MACHALI, miaka 31, Muha, Mbunge wa Kasulu Mjini kupitia NCCR – Mageuzi
wakati anaelekea nyumbani kwake
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Bw.David. A. Misime alisema Tukio hilo limetokea tarehe 20/06/2013 majira ya 19.00 hrs katika eneo la Area ‘E’ katika Manispaa ya Dodoma
“alikutana
na vijana wanne (4) walikouwa amesimama katikati ya barabara akapiga
honi lakini hawakupisha. Aliamua kuwauliza “Jamani mnasimama katikati ya
barabara si nitawagonga?” Nao wakamjibu: “Wewe si unajifanya mtto wa
Mbunge, tutakupiga sasa”. Alisisitiza Kamanda Misime
Kamanda Misime alisema Mheshimiwa alipojaribu
kupita vijana hao walipiga gari lake. kitu ambacho kilimfanya ashuke
ili atazame kama gari hilo limepata uharibifu.wowote, ndipo vijana hao
wakaanza kumshambulia kwa ngumi na mateke huku naye akijitahidi
kujihami.
Hata
hivyo Bw.Misime alisema, walitokea vijana wawili (2) na kumsaidia.
Mheshimiwa mbunge ambapo kijana mmoja kati ya waliokuwa wanamshambulia
Mheshimiwa Machali ‘alimng’ata’ mgongoni kijana aliyekuwa anamsaidia
Mheshimiwa Mbunge.
Bw.
Misime alisema Watuhumiwa baada ya kuona wamezidiwa nguvu walitimua
mbio. Ambapo pia Mheshimiwa Machali aligundua kuwa simu yake ya mkononi
wameondoka nayo vijana hao.
Kamanda
David. A. Misime alisema jeshi la Polisi mkoani Dodoma lilifanya Msako
mkali ulifanyika usiku wa manane ambapo watuhumiwa wawili (2)
walikamatwa ambao aliwataja kuwa ni JEREMIA LAWRENT MKUDE@ JERRY, Miaka
18, Mkaguru Mkazi wa Chaduru, Manispaa ya Dodoma. aliyekutwa akiwa na
jeraha usoni alilopata wakati anapambana na Mheshimiwa Mbunge na vijana
waliokuwa wanamsaidia.
Kamanda
huyo wa Polisi Mkoa wa Dododoma alimtaja mtuhumiwa mwingine
anayeshikiliwa na jeshi la polisi kuwa ni CHARLES CHIKUMBILI, Miaka
22, Mkulima, Mkazi wa Swaswa, katika Manispaa ya Dodoma.
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Bw. David Misime alisema askari walipowafanyia upekuzi wa mwili watuhumiwa usiku huo wa manane wamekutwa na misokoto miwili (2) ya bhangi
Post a Comment