Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAZIRI PINDA ALIA NA UDHAIFU WA WATENDAJI SERIKALINI


WAZIRI mkuu  Mizengo Pinda amesema udhaifu mkubwa uliopo katika serikali ni kukosekana kwa  umakini wa ufuatiliaji na usimamizi imara, wa miradi inayoibuliwa kwa lengo la kuwainua wananchi, hali inayosababisha miradi kutokamilika na dhamani ya fedha kutoendana na miradi.


Pinda ametoa kauli hiyo jana mjini Moshi, wakati akizinduwa mradi waUimarishaji wa Miji 18 za  Tanzania bara, ulifadhiliwa na benki ya dunia kwa lengo la  kuimarisha uwezo wa kutekeleza majukumu ya Halimashauri na miji ili kutoa huduma bora kwa wanachi.

Alisema tatizo kubwa lililopo ndani ya serikali ni kukosena kwa ufuatiliaji makini wa miradi, hali inayosababisha miradi kukamilika chini ya kiwango, pamoja na dhamani fedha kutoendana na kazi husika. 

Amesema baadhi ya watendaji wa halimashauri wamekuwa mabingwa wa kutafuta visingizio pindi mradi unaposhindwa kukamilika kwa wakati, au chini ya kiwango, kwa kujitetea vifaa viliibiwa, na kudai uzembe kama huo hatokubalina nao katika mradi huu wa miji.

Waziri panda amesema serikali haitakuwa tayari kusikiliza vigezo wala sababu zozote za kukwamisha kazi ya mradi huo, wala kufumbia macho uzembe  au ubadhilifu wa fedha au vifaa utakaosababisha kazi kukwama au kutekelezwa chini ya kiwango.

Amesema litakuwa jambo la kusikitisha na kusononesha endapo itatokea mojawapo ya halimashauri kati ya 18 zilizochaguliwa, kuishia njiani bila kukamilisha mradi huo kwa muda wa miaka mitano.

Amebainisha mradi huo utaongeza imani kwa wananchi na kuvutia wadau wengine kushirikiana na halimashauri za hapa nchini, hivyo wakurugenzi wanatakiwa kuomba ushauri kwa viongozi pale wanapoona kuna dalili za vikwazo ambavyo vinaweza kusababisha ucheleweshaji wa utekelezaji wa mradi.

Pinda amesema njia ya kufikia mafanikio ya mradi huo ni kuwepo kwa uwajibikaji, utunzani wa miradi iliyokamilika, ukusanyaji wa mapato, pamoja na ushirikishwaji wa wananchi kwa kushirikisha ngazi zote ikiwa ni pamoja na taarifa za utekelezaji wa mradi ziwekwe wazi.

Kwa upande wake Kaimu Katibu mkuu ofisi ya Waziri mkuu (TAMISEMI), Jumanne Sangini alisema mradi huo unatekelezwa kwa ufadhili wa benki ya dunia kwa garama ya zaidi ya Sh bilioni 400 kwa miji ipatayo 18 ya hapa nchini Sangini alisema mradi huo unalenga kuimarisha halmashauri za miji katika maeneo matano ili ziweze kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi, moja ikiwa ni kuboresha mfumo wa mipango miji na ukusanyaji wa mapato ya ndani,.

Ametaja maeneo mengine ya mradi utakapolenga kuwa ni uboreshaji wa mifumo ya udhibiti wa fedha manunuzi ya maswala ya mazingira, mfumo wa utekelezaji utunzaji wa miundombinu kwa ajili ya huduma za jamii, na kuboresha uwajibikaji.

Mwandishi: Arnold Swai, Moshi-Kilimanjaro
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top