Habari za kuaminika kutoka kwa chanzo cha
karibu na uongozi wa klabu wa Yanga ni kwamba mabingwa hao watetezi wa kombe la
Kagame hawatoenda kushiriki michuano hiyo mwaka huu iliyopangwa kuanza hivi
karibuni huko Darfur Sudan.
Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya
serikali kupitia wizara ya mambo ya nje ya Tanzania kusema kwamba haioni busara
kwa vilabu kwenda Darfur kwa sababu eneo hilo bado halina usalama wa kutosha -
kauli iliyopelekea mwenyekiti wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage kusema kwamba
timu yake haitokwenda Darfur kushiriki michuano hiyo mwaka huu.
Kwa mujibu wa CECAFA na chama cha soka cha
Sudan ni kwamba michuano hiyo itachezwa kwenye eneo lililo salama na lenye
ulinzi mkubwa hivyo timu hazihitaji kuwa na wasiwasi juu ya usalama wao pindi
watakapoenda kushiriki michuano hiyo mapema mwezi ujao.
Hatua ya Yanga kujitoa inazidi kuongeza idadi
ya vilabu ambavyo vimesema ikiwa michuano hiyo itafanyika Darfur basi
havitashiriki Kagame Cup mwaka huu, vilabu vikubwa vya Sudan AL Hila na El
Merreikh, Tusker ya Kenya na Simba SC vyenyewe vilishatangaza uamuzi wa
kutokwenda Darfur kwa ajili ya michuano hiyo.


Post a Comment