Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF) jana walifanya ziara katika ofisi za Makao Makuu ya Mfuko huo kwa lengo
la kutembelea ofisi hizo na kuangalia mazingira ya kazi.
Mkurugenzi wa Uendeshaji, Eugen Mikongoti akitoa
maelezo ya namna ya kuhifadhi kumbukumbu za wanachama katika kituo cha kisasa
cha Mfuko huo.
Wajumbe hao wakipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa NHIF
namna ya upatikanaji wa haraka wa kumbukumbu za wanachama zinazohifadhiwa katika
kituo hicho.
Wajumbe wakiendelea kujifunza zaidi katika kituo cha
kuhifadhia kumbukumbu.
Mkurugenzi Mkuu Emanuel Humba (wa nne kulia) akifafanua
jambo wakati wa ziara hiyo
*****
Wajumbe walioteuliwa hivi karibuni wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Balozi Ali Mchumo, Mwanaidi Mtanda, Ezekiah Oluoch, Donan Mmbando, Mohamed Mohamed, Lydia Choma, Mohamed Hashim, Charles Kajege na Emanuel Humba ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo.
Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Raphael Mwamoto walipozuru Makao Makuu jana.


Post a Comment