Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga wameamua
kuboresha zaidi safu yao ya ulinzi baada ya kumsajili kipa Deo Munishi maarufu
kama Dida.
Mmoja wa ‘majembe’ ya Yanga katika suala la
usajili, Abdallah Bin Kleb amethibitisha kumsajili Dida.
“Kweli tumemsajili Dida, tumempa mkataba wa miaka
miwili na lengo letu ni kuimarisha safu ya ulinzi.
“Hivyo Dida atashirikiana na Barthez kuimarisha
ulinzi katika lango la Yanga,” alisema Bin Kleb.
Dida alikuwa kipa wa Azam FC, lakini timu yake
hiyo haikumpa mkataba baada ya kuingia katikam mgogoro kutokana na shutuma za
kupanga matokeo.
Azam FC ililifikisha suala hilo kwa Taasisi ya
Kupamabana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) na baada ya muda majibu yalitoka Dida na
wenzake Erasto Nyoni, Agrey Morris na Said Morad hawakuwa na
hatia.
Kabla ya kutua Azam FC, Dida alikuwa kipa namba
moja wa Mtibwa Sugar aliyojiunga nayo akitokea Simba alikokuwa kipa namba tatu
chini ya Juma Kaseja na Ally Mustapha ‘Barthez’.
Maana yake Dida amekutana na Barthez kwa mara
nyingine tena, safari hii wakiwa makipa wa Yanga.
Post a Comment