Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete
...............................................................................................................................................
WAKAZI wa Ileje wanaoishi Mkoani Mbeya wamesema kuwa endapo suala la kugawa Mkoa Mpya halitabadilishwa wananchi wa wilaya hiyo wamesema kuwa hiyo itakuwa CCM kwa heri kulikoni kuhamia Mkwajuni ni bora kwenda Malawi ambako walikuwa wakipatiwa huduma za kiafya toka mwaka 1975.
Kauli hiyo inakuja baada ya taarifa ya mapendekezo Sekretarieti ya Mkoa kuwa Makao Makuu yawe Mkwajuni wilayani Chunya na Mkoa uitwe Songwe.
Kauli hiyo ya pamoja imetolewa jana na wananchi hao walipokutana kujadili na kutoa tamko lao mkutano ambao ulifanyika katika ukumbi wa hoteli ya Kiwira Moteli uliopo Jijini hapa.
Walisema kuwa kama wananchi wa Ileje hawako tayari kwenda Mkwajuni kama Rais Kikwete ataridhia maamuzi ya sekretarieti ya Mkoa huo hivyo tunapoinga na tutaendelea kupinga kwani tunakuwa kama tunaburuzwa.
Mmoja wa wakazi wa Ileje aliyekuwepo katika Mkutano huo Hosea Cheyo alisema kuwa kila sehemu wanapogawa utawala lazima pande fulani ziumie kwa eneo la wananchi wa Ileje wamepata maumivu makali sana.
“Katika hili tunaomba Rais Kikwete aone umuhimu wa kubadilisha mapoendekezo ya Kamati ya ushauri wa Mkoa kwamba makao yasiwe Mkwajuni badala yake yasogezwe hata Wilaya ya Mbozi kwasababu mwanzoni wana ileje walikuwa wanafuata huduma makao makuu ya zamani ya Mkoa ambayo ni Mbeya ambako tulikuwa tukitumia kilometa 215 na sasa huko Mkwajuni tutalazimika kutumia kilometa 315”alisema Mkazi huyo.
Hata hivyo alisema kuwa ili jambo hili liweze kukaa vema hakuna kwa Rais Kikwete atakapopata mapendekezo hayo ya kamati ya ushauri afikirie kwa kina jambo hilo na asiafiki mapendekezo hayo kwani ni tatizo kwa wana ileje.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Wana Ileje hao Said Ngondo alisema kuwa wao kama wana ileje wamepinga makao makuu kuwa Mkwajuni kwani kitendo hicho kitafanya wana ileje kuendelea kuwa na maisha duni kutokana na umbali wa Makao makuu ulipo.
“Sisi tunachotaka Makao makuu yawe Mbozi kama tulivyokuwa tumependekeza awali kwa hili la Mkwajuni tunapinga “alisema.
Akitoa Tamko kwa waandishi wa habari jana Mbunge wa Jimbo la Ileje Aliko Kibona alisema kuwa kaama makao makuu mbozi basi9 suala hilo litaleta shida sana kwani wao hawawezi kufuata kamati ya ushauri ya Mkoa na kwa kupendekeza hili naona hawaitakii mema CCM.
“Kisiasa jambo hili nasema kuwa nimekuwa nikipata ujumbe mfupi wa maneno kutoka kwa wana ileje ukisema CCM kwa heri maana sera ya CCM kuwasilikiza wanyonge ambao ndo wananchi pamoja na kusogeza huduma za maendeleo karibu”alisema Mbunge huyo.
Awali katika kikao cha Kamati ya ushauri ya Mkoa kilichofanyika hivi karibuni katika mapendekezo hayo Mkoa utaundwa na wilaya za Mbozi, Chunya,Ileje,Momba na Makao Makao makuu yatakuwa Mkwajuni.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Mariam Mtunguja katika kikao hicho alisema baada ya kujadili kwa kina Sekretarieti iliona kuunganisha wilaya hizo ambazo kimsingi zinaweza kukizi vigezo vya kuunda Mkoa Mpya kutokana na vigezo vilivyoa ainishwa kutoka serikalini.
Moja ya vigezo hivyo ni idadi ya watu pamoja na kigezo cha Kijografia alisema kuwa baada ya watalaamu kuangalia waliona ni vema kuifanya Mkwajini kuwa Makao Makuu ya Mkoa.
Alisema kuwa Mkoa katika mapendekezo hayo Mkoa utaundwa na wilaya za Mbozi, Chunya,Ileje,Momba na Makao Makao makuu yatakuwa Mkwajuni.
Alisema baada ya kujadili kwa kina Sekretarieti iliona kuunganisha wilaya hizo ambazo kimsingi zinaweza kukizi vigezo vya kuunda Mkoa Mpya kutokana na vigezo vilivyoa ainishwa kutoka serikalini.
Hoja ya kuugawa Mkoa iltolewa na Rais Jakaya Kikwete siku ya sikuu ya wafanyakazi duniani Meimosi ambapo mwaka huu kitaifa ilifanyika Mkoa Mbeya.
Akihutubia wananchi wa Mbeya Kikwete alisema amepokea taarifa kutoka Sekretarieti ya Mkoa kuomba Mkoa wa mbeya una kila sababu ya kuugawa na Kuiagiza ofisi ya Mkoa kuanza kujadili namna ya kuugawa.
CREDITS: Na Esther Macha wa matukio daima.com ,Mbeya
mwisho.
Post a Comment