Mwenyekiti wa Chama Cha
Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema, pichani, amechaguliwa na mkutano
Mkuu wa Kituo cha Demokrasia nchini (TCD), kuwa Mwenyekiti mpya atakayekiongoza
kwa mwaka mmoja.
Uchaguzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki na wajumbe
wapatao 25 ambapo Mrema alipita bila kupingwa na kupewa nafasi hiyo baada ya
mtangulizi wake, James Mbatia, kutoka NCCR-Mageuzi kumaliza muda
wake.Katika mkutano huo
uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo, alichaguliwa
kuwa Makamu Mwenyekiti wa kituo hicho.
Akizungumza muda mfupi baada ya
kuchaguliwa, Mrema alisema amefarijika kuwa bosi katika kituo hicho kinachoundwa
na vyama sita vyenye wawakilishi bungeni kikiwamo Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Chama cha Demokrasia na Maendeleo, TLP, Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi
na UDP.
Aidha, Mrema alisema yeye na viongozi wenzake wataendeleza yale
yote yaliyofanywa na watangulizi wao kwa lengo moja la kujenga siyo
kubomoa.
Loading...
Post a Comment