Caylee Anthony miaka 2, enzi za uhai wake
Na Swahili TV
Watu wengi wamepigwa na butwaa kwa yalitokea katika kesi ya mauaji iliyorindima kwa zaidi ya mwaka mmoja katika vituo mbalimbali vya habari ambapo George Zimmerman alishatikiwa na Serikali kwa kosa la kumuua kwa kumpiga risasi kijana mweusi Trayvon Martin miaka 17 aliyekuwa akitembea katika mtaa anakoishi Zimmerman mnamo Februari 26, 2012 katika mji wa Sanford, Florida.
Kesi hii ilitawaliwa na hisia za kibaguzi wa rangi miongoni mwa watu weusi na weupe raia wa Marekani. Tofauti na matarajio ya wengi, George Zimmerman ameibuka mshindi katika kesi hii ya mauaji!!
Mauaji ya kikatili ya Trayvon Martin miaka 17, yalipelekea maandamano makubwa ya watu weusi pamoja na wapigania haki za kiraia hapa nchini yaliyoongozwa na Mchungaji Al Sharpton mwanaharakati maarufu nchini Marekani.
Katika kesi hii mtazamo wa wengi ulitegemea Zimmerman kukutwa na hatia, lakini jana jumamosi julai 13,2013 mahakama ya Sanford, Florida imeshangaza dunia kwa kumwachia huru bwana George Zimmerman ambaye kama alivyojiita sungusungu wa mtaa wa kujitolea.
Hii ni mara ya pili kwa mahakama katika jimbo la Florida kuacha midomo wazi dunia! Hapo nyuma mwaka juzi Julai 5 , 2011 katika kesi iliyozizima dunia nzima, mahakama ya Orange, Orlando Florida; ilimwachia huru mwana mama Case Anthony aliyeshitakiwa kwa kosa la kumuua mwanae wa kumzaa Caylee Anthony aliyekuwa na umri miaka 2.

Post a Comment