Wanafunzi nchini Kenya wakiwa darasani
Serikali nchini Kenya imetangaza kufungwa kwa
shule zote za msingi za umma kufuatia mgomo wa walimu ulioingia wiki ya nne
sasa.
Waziri wa elimu prof Prof. Jacob Kaimenyi
amesema kuwa shule hizo zitabakia kufungwa kwa muda usiojulikana. Ameshutumu
walimu akisema kuwa mgomo wao ulikuwa kinyume cha sheria.
Zaidi ya walimu laki mbili na arobaini wamesusia
kutoa mafunzo kwa wanafunzi wakidai nyongeza ya asili mia mia tano ya mishahara
waliyoahidiwa na serikali mwaka wa 2007.
Pia wanataka kuongezewa marupurupu ya usafiri,
ya nyumba na matibabu. Serikali imesema kuwa wazazi wataarifiwa juu ya siku ya
kufunguliwa tena shule.
Waziri huyo wa elimu Pro. Kaimenyo amesem akuwa
wizara yake itafanya mipango maalum kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la nane
wanaotarajiwa kufanya mtihani wao wa kitaifa chini ya miezi minne ijayo
Post a Comment