STRIKE


Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limetumia helikopta kushambulia ngome za waasi wa M23 kwa siku ya tatu mfululizo katika mapigano yaliyoibuka upya karibu na mji wa mashariki wa Goma.
Jeshi hilo limesema kuwa waasi walionekana wakikimbia kutokana na mashambulizi hayo.
Kanali wa jeshi hilo Mustapha Mamadou ameema walikuwa wakijibu uchokozi ulioanzishwa na waasi.
Hata hivyo taarifa iliyotolewa na jeshi la Afrika Kusini mbalo lina askari mjini Goma, imesema mashambulizi ya jeshi dhidi ya waasi, ambayo yalianza Jumapili, yalikuwa yamepangwa mapema.
Jeshi la serikali limesema kuwa limewasogeza nyuma waasi kwa umbali wa kilometa 3.
Mapigano hayo yamekwamisha mazungumzo kati ya Kinshasa na M23 ambayo yamekuwa yakiendelea katika mji mkuu wa Uganda, Kampala.
Kongo imeishutumu Rwanda kuunga mkono waasi wa M23 katika mapigano hayo na Rwanda imeishitaki Kinshasa kushirikiana na waasi wa FDLR.-DW.