Watoto saba ambao ni raia wa Burundi na Rwanda
ambao walikamatwa wakati walipokuwa wakisafirishwa kutoka Burundi kuja Tabora
kwa ajili ya kuuzwa
watumikishwe katika mashamba ya tumbaku,Watoto
hawa walikamatwa eneo la Ulyankulu wilayani Kaliua wakiwa na tajiri yao ambaye
amefahamika kwa jina la Emmanuel John(22) ambaye pia ni raia wa Burundi.
Watoto wakiwa mahakama ya hakimu mkazi Tabora
wakisubiri kuingia mahakamani kutoa ushahidi baada ya mtu aliyekuwa
amewasafirisha kwa lengo la kutaka kuwauza kukamatwa na kufikishwa Mahakamani
kujibu shitaka la kuwasafirisha kwa nia ya kuwafanyia biashara na kuingia nchini
kinyume cha sheria.
Afisa na Mwanasheria wa Idara ya Uhamiaji mkoa
wa Tabora akiwaongoza watoto hao kuingia chumba cha mahakama ya hakimu mkazi
Tabora kwa ajili ya kutoa ushahidi dhidi ya Emmanuel John.
RAIA wa Burundi, Emmanuel John
(22),aliyekamatwa akituhumiwa kusafirisha watoto,amefikishwa katika Mahakama ya
Mkoa waTabora akikabiliwa na Mashitaka mawili moja likiwa ni la kuingia nchini
kinyume cha sheria na kusafirisha binadamu kwa lengo la kutaka kuwauza.
Mbele ya Hakimu Mkazi Bw. Jackton
Rushwela,Wakili wa Serikali Bw.Iddi Mgeni, alimsomea mshitakiwa mashitaka hayo
ambapo alikiri kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria huku kosa la pili la
kuwasafirisha watoto hao saba akijaribu kutaka kuficha ukweli.
Kutokana na kukiri kosa la kwanza, Hakimu
Rushwela alimhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya sh 100,000.
Hata hivyo,mshitakiwa huyo Emmanuel John pamoja
na kuiomba mahakama impatie fursa ya kumtaarifu mkewe aliyeko huko nyumbani kwao
nchini Burundi kwa njia ya simu au apewe nafasi ya kuuza simu yake ya mkononi
aweze kulipa faini hiyo kwa nia ya kutaka kujinasua na adhabu ya kifungo hicho
cha mwaka mmoja lakini mahakama haikuwa tayari kutekeleza hilo.
Kuhusu shitaka la kusafirisha binadamu,upande
wa mashitaka ulidai mshtakiwa alikamatwa na maofisa wa Idara ya Uhamiaji
akiwasafirisha watoto Ndayisenga Batiliza(13), Ndakusenga Emmanuel(15),
Nimbonajile Nagenda(13), Yazid John(15), James Justus(14) na Samson
Banteke(17).
Baadhi ya watoto hao walitoa ushahidi walidai
walisafirishwa na mshitakiwa Emmanuel John kutoka nchini Burundi na Rwanda hadi
walipokamatwa eneo la Ulyankulu wilayani Kaliua.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 25, mwaka huu
itakapoendelea tena kusikilizwa kwa mashahidi wengine kutoa ushahidi wao.





Post a Comment