Loading...
Home »
Unlabelled »
WATU 181 WAMEUAWA KATIKA MAPIGANO YA KIKABILA NCHINI KENYA

Watu 181 wameuawa na wengine 217 wamejeruhiwa katika mapigano ya kikabila yaliyotokea kuanzia mwezi Januari mwaka huu nchini Kenya. Ripoti iliyotolewa na ofisi ya uratibu wa mambo ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA imesema mapambano hayo pia yamesababisha watu zaidi ya elfu 52 kukimbia makazi yao. Msemaji wa Ocha Bw. Matthew Conway amesema serikali ya Kenya, chama cha msalaba mwekundu na jumuiya zisizo za kiserikali wanatoa msaada kwa watu walioathiriwa.
Kwa mujibu wa takwimu za OCHA wahanga wengi zaidi walitokea kwenye mapambano ya kikabila kati ya jamii za wa-garre na wa-degodia. Hata hivyo OCHA imesema serikali imetuma wanausalama katika eneo hilo na kuanzisha mpango wa kunyang'anya silaha.
on Sunday, July 14, 2013
Post a Comment