Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

HII HAPA RATIBA YA MAZISHI NA WASIFU ( RISALA ) YA MAREHEMU NDG JOHN SHILATU



RATIBA YA MAZISHI YA NDG. JOHN SHILATU 27 JULAI, 2013

A.
MUDA
TUKIO
MHUSIKA/WAHUSIKA
1.
02:00 – 03:00 ASUBUHI
KUPATA KIFUNGUA KINYWA
WAFIWA NA WAGENI
2.
03:00 – 05:00
KWAYA
VIKUNDI NA WAGENI
2.
05:00 – 06:00
CHAKULA
WOTE
3.
06:00 – 06:30 MCHANA
MWILI KUWASILI NYUMBANI
WAGENI/ FAMILIA YA MAREHEMU
4.
06:30 – 7:00 MCHANA
IBADA
(NYUMBANI)
WOTE
5.
07:00 – 07:15 MCHANA
WASIFU WA MAREHEMU
RODRICK
6.
07:15 – 07:20 MCHANA
NENO (A EUOLOGY)KUTOKA WATOTO WA MAREHEMU        NDUGU SHILATU
HELLEN
7.
07:20 – 07:30 MCHANA
NENO KUTOKA MCHUNGAJI
PASTOR JEREMIAH
8.
07:30 – 07:40 MCHANA
NENO KUTOKA CHAMA CHA MAPINDUZI
MWENYEKITI
9.
07:40 – 08:40 MCHANA
KUTOA HESHIMA ZA MWISHO (NYUMBANI )
WOTE
10.
08:40 – 09:30 ALASIRI
KUELEKEA MAKABURINI
WOTE
11.
09:30 - 10:30 ALASIRI
MAZISHI
WOTE
12.
10 :30 JIONI
SALAMU ZA RAMBIRAMBI
WAHUSIKA

 
WASIFU WA MAREHEMU NDG. JOHN SHILATU
Aliyekuwa Baba, Babu, Mwalimu, Mwanansiasa na Kiongozi wetu Ndugu John Steven Shigemelo Shilatu alizaliwa Tarehe 24/06/1951 katika Kata ya Kisesa, Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza akiwa ni Mtoto wa pili (2)  kati ya Watoto Watatu (3) ya familia ya Mzee Steven Shigemelo Shilatu na Mama Teje Mwanangeleja ambao wote ni kabila la Wasukuma wa mkoani Mwanza.
 
ELIMU:
Elimu ya Msingi: Mwaka 1959 alianza darasa la Kwanza katika shule ya msingi ya Bukandwe iliyopo katika kata ya Kisesa ambapo alisoma mpaka darasa la nne mwaka  1962 ambapo alihamia katika shule nyingine ya Msingi ya Bujora iliyopo Kata ya Kisesa ambapo alisoma darasa la tano mpaka darasa la nane kuanzia mwaka 1963 hadi mwaka 1966.
Elimu ya Sekondari: Mara baada ya kumaliza elimu ya msingi alifanikiwa kuwa Mwanafunzi wa pekee kati ya wote waliomaliza kufaulu na kupata fursa ya kujiunga na shule ya sekondari ya Bwiru iliyopo katika kata ya Kitangili Mwanza mjini ambapo alisoma kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne kuanzia mwaka 1967 hadi 1970.
MAFUNZO:
Mara ya kumaliza elimu ya sekondari alifanikiwa kufaulu tena na kupata fursa ya kujiunga na chuo cha Ualimu cha Chang’ombe kilichokuwa kikiitwa Chang’ombe Teacher’s Training College kuanzia mwaka 1971 mpaka mwaka 1972.
Baada ya kumaliza digrii (Shahada) yake ya Ualimu alienda kupata mafunzo ya Kijeshi  ya muda wa miezi sita katika chuo cha kijeshi cha Mafinga - Iringa kilicho chini ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) mnamo 1971 kwa mujibu ya utaratibu na sheria zilivyokuwa kabla ya kuajiliwa na Serikali.
KAZI:
Kutokana na ufaulu wake kuwa mkubwa sana akiwa chuoni, Mnamo tarehe 06.11.1972 kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo  alipata fursa ya kupata kazi ya ualimu ambapo aliteuliwa kuwa Mwalimu Mkuu wa kwanza kabisa Mwafrika katika shule ya Msingi ya Chang’ombe.
Kutokana na utendaji kazi wake bora wa ufauluishaji cha hali ya juu aliipatia shule ya Msingi ya Chang’ombe heshima ya kipekee kuwa shule bora ya msingi kitaifa kutokana na ufauluishaji bora na nidhamu bora aliyofanikiwa kuwajengea Walimu na Wanafunzi wa shule ya msingi ya Chang’ombe.
Alifanikiwa kuwa Mwalimu mkuu kwa takribani miaka 14 ya kuanzia mwaka 1972 hadi mwaka 1984
Mnamo tarehe 19/08/1998 alirudishwa tena kwenye kazi yake ya ualimu na kuwa Mwalimu wa shule ya msingi ya Chang’ombe na baadae shule ya Msingi ya Mtoni alipostaafu rasmi Ualimu mnamo Julai, 2011.
 
UONGOZI:
Katika enzi za uhai wa maisha yake, Marehemu John Shilatu alionyesha kipaji kikubwa cha uongozi tangu akiwa shule ya msingi na kpaji chake kilikuja kuonekana kitaifa mara baada ya kuwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Chang’ombe ambapo mnamo tarehe 11/01/1984 ilipelekea chama tawala Chama Cha Mapinduzi kumuazima kutoka katika Ualimu Mkuu na kwenda kufanya shughuli mbalimbali za kiuongozi ndani ya chama ambapo aliteuliwa kuwa Mkuu wa Idara Huduma za Umma CCM katika Wilaya ya Temeke kuanzia mwaka 1984 hadi mwaka 1987.
Mwaka tarehe 22/12/1987 alipanda daraja na kuwa Katibu wa Idara ya Huduma za Umma CCM katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo alidumu na nafasi hiyo kwa muda wa miaka mitano mpaka mwaka 1992.
Mwaka 1988 mpaka mwaka 1994 alifanikiwa kuwa Diwani wa jiji la Dar es Salaam ambapo alifanikiwa pia kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu na Utamaduni Halmashauri ya Jiji Dar es Salaam.
Mwaka 1989 mpaka mwaka 1991 aliteuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Kariakoo Masoko
Mnamo tarehe 28/02/1995 aliyekuwa Rais wa awamu ya pili Dk. Alhaji Ali Hassan Mwinyi akishirikiana na Waziri Mkuu Cleopa David Msuya (wa kipindi hicho)alimteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga.
Mwaka 1997 alipadilishwa kituo cha Kazi na kupelekwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukombe iliyopo mkoani Shinyanga mpaka mwaka 1998.
Mnamo tarehe 26/08/1997 aliteuliwa kuwa Kiongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Bukombe mpaka mwaka 2002.
Mnamo  tarehe 10/03/1998 Rais Benjamin Mkapa alisikiliza ushauri dhaifu wa aliyekuwa Waziri Mkuu Fredrick Sumaye (wa kipindi hicho) na kusitisha wadhifa wake wa Ukuu wa Wilaya.
Pia alishawahi kuwa Mjumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM (W) Temeke kwa miaka 20 mfululizo.
Halikadhalika alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa miaka 25 mfululizo.
Pia alikuwa Mjumbe wa Halmaushauri kuu ya Taifa (NEC) kwa muda wa miaka 10 mfululizo.
NDOA NA FAMILIA
Mnamo mwaka 1980 alifanikiwa kufunga ndoa ya pekee na Bernadina Joseph Makere, ndoa ambayo alidumu nayo mpaka umauti unamkuta
 Kwa takribani miaka 14 Ndugu John Shilatu alikuwa akisumbuliwa na maradhi mbalimbali na umauti ulimkuta kutokana na shinikizo la damu ya kupanda ghafla usiku wa saa 8 tarehe 23/07/2013 na kupelekea mishipa ya damu kupasuka na kuvujisha damu ubongoni na hatimaye umauti kumkuta saa 9 alasiri ya tarehe 23/07/2013.
Marehemu Ndugu John Steven Shigemelo Shilatu ameacha mjane mmoja; Watoto watano ambao ni Benigna Shilatu (Akijiwe-Sebha), Emmanuel Shilatu (Chei au Buyegu), Geofrey Steven (Nondeji), Gerald John (Ntongeji) na Digna John (Wakubu-Shosha); na Mjukuu mmoja aitwaye Jayden.
Daima tutakukumbuka kwa malezi bora, upendo wa dhati uliokuwa nao kwa kila mtu, Ualimu uliotukuka, ucheshi na nasaha ulizotuachia.
MAVUMBINI TULITOKA NA MAVUMBINI TUTARUDI,
 
JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
 
Amen!!




Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top