Mshambuliaji wa timu ya Taifa Stars, Mrisho Ngassa (katikati) akijaribu
kuwatoka mabeki wa Uganda, katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza
fainali za CHAN 2014. Uganda ilishinda 1-0. Picha na Michael Matemanga.
KIWANGO cha chini kilichoonyeshwa na wachezaji wa Taifa Stars juzi dhidi ya timu ya taifa ya Uganda, kimewavunja moyo baadhi ya wapenzi wa soka hapa nchini na kujikuta wakipoteza matumaini ya kuiona timu hiyo ikifuzu kushiriki katika fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za nyumb
ani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
KIWANGO cha chini kilichoonyeshwa na wachezaji wa Taifa Stars juzi dhidi ya timu ya taifa ya Uganda, kimewavunja moyo baadhi ya wapenzi wa soka hapa nchini na kujikuta wakipoteza matumaini ya kuiona timu hiyo ikifuzu kushiriki katika fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za nyumb
ani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Hata hivyo kocha mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen
amewataka kuwa wavumilivu kwani lolote linaweza kutokea katika mechi ya
marudiano itakayofanyika nchini Uganda wiki mbili zijazo.
“Suala ni kwamba tulitengeneza nafasi tukashindwa
kuzitumia, katika mechi ya marudiano tunatakiwa kutengeneza nafasi na
kuzitumia kwani mpira ni magoli,” alisema kocha Poulsen.
Katika mechi hiyo ya marudiano, Taifa Stars ambayo
juzi ililala kwa bao 1-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa
Taifa, inatakiwa kushinda zaidi ya mabao 2-0 ili iweze kujihakikishia
mazingira mazuri ya kufuzu kushiriki fainali hizo za CHAN
zitakazofanyika Afrika Kusini ambazo zitakuwa za tatu kufanyika tangu
kuanzishwa kwake.
Katika mechi ya juzi dhidi ya Uganda, wachezaji wa
Stars walicheza chini ya kiwango tofauti na walivyocheza dhidi ya
Morocco na Ivory Coast wiki chache zilizopita wakati wakitafuta tiketi
ya kufuzu kushiriki Fainali za Kombe la Dunia 2014.
Nguvu na kuchoka
Wachezaji wengi wa Taifa Stars katika mechi hiyo
walionekana kutokuwa na nguvu kabisa, pia walichoka mapema ukilinganisha
na wapinzani wao.
Mara nyingi kila walipokuwa wakishindana kuwania
mpira wachezaji wa Uganda walikuwa wakiibuka na ushindi ingawa walikuwa
hawatofautiani sana kwa maumbo.
Hata hivyo kocha mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen
alipoulizwa juu ya hali hiyo alisema kuwa pengine imechangiwa na
wachezaji wengi wa kikosi hicho kuwa katika mfungo wa mwezi mtukufu wa
Ramadhani.
Kusoma mchezo
Hilo pia lilikuwa ni tatizo kwa wachezaji wa Stars
kwani hakukuwa na uwezo wa kuusoma mchezo na kutafuta mbinu mbadala za
kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo huo tofauti na ilivyo
kuwa kwa wenzao wa Uganda ambao kipindi cha pili walibadili mfumo na
kupata bao la mapema.
Umakini wa washambuliaji CHANZO MWANANCHI
Post a Comment