Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

IGP SAIDI MWEMA AWAANGUKIA VIONGOZI WA DINI, AWAOMBA WAHIMIZE UTII WA SHERIA.

 


Inspekta jenerali wa Polisi ,Said Mwema.

MKUU wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema, amewataka viongozi wa dini kushiriki kikamilifu kampeni ya kuhimiza utii wa sheria bila shuruti, kama sehemu ya mapambano dhidi ya uhalifu na uvunjifu wa amani nchini. IGP Mwema, aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Baraka za Utii bila Shuruti Mkoa wa Kilimanjaro.

Kampeni hiyo, inaendeshwa na viongozi wa madhehebu yote ya dini kwa kushirikiana na polisi.

IGP Mwema ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo uliofanyika jana katika Viwanja vya Mashujaa mjini Moshi, alisema katika taarifa yake iliyosomwa kwa niaba yake na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, kuwa viong

ozi hao wana nafasi kubwa ya kuhamasisha amani au kuhimiza uvunjifu wake kutokana na kusikilizwa zaidi na waumini wao.

“Viongozi wa dini, sisi kama Jeshi la Polisi tunatambua mchango wenu katika jamii, uwezo mlionao katika juhudi za kuhamasisha amani ya nchi, inabidi sasa tufike mahala tushirikiane kuhamasisha amani na usalama wa wananchi wetu, kwa sababu mnasikilizwa vizuri zaidi,” alisema IGP Mwema.

Alisema hayo ni matokeo ya mikakati na malengo ya polisi, kushirikiana na wananchi kutunza, kulinda na kudumisha amani kwa nia ya kutokomeza uhalifu.

Alisema hayo yote, hayataweza kufanikiwa kama jamii yenyewe haitaamua kujihusisha na harakati za kujilinda.

Kwa upande wake, Mratibu wa Kampeni ya Baraka za Utii wa Sheria bila Shuruti Taifa, Mchungaji Zabedius Isaya alisema uzinduzi huo, ni mwendelezo wa juhudi za kanisa kuhakikisha waumini wake wanakuwa watiifu kwa mamlaka zote.

Naye Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Aggrey Mwanri alisema Serikali katika kutambua umuhimu wa amani ya nchi, imeamua kuwashirikisha wananchi wote katika juhudi za kulinda amani iliyopo. chanzo Mtanzania
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top