wanawake wafanyakazi Saudi Arabia
Saudi Arabia imetangaza sheria mpya
zinazotarajiwa kuwapa haki zaidi mamilioni ya wafanyikazi wa nyumbani.
Miongoni mwa sheria hizo ni kuwa waajiri watoe
haki kamili kwa wafanyikazi zao.
Kwa upande wa wafanyakazi hao watahitajika
kuwaheshimu waajiri wao na kuheshimu dini ya Kiislamu.
Kumekuwepo malalamiko mengi ya unyanyasaji
unaofanyiwa wafanyikazi hao katika mikono ya waajiri.
Masaibu ya wanawake wanaofanya kazi kama
wasaidizi wa nyumbani nchini Saudi Arabia yamezua hamaki nyingi miongoni mwa
wanaharakati wa haki za binadamu kwa miaka mingi.
Katika tukio baya zaidi, baadhi yao hupigwa na
waajiri wao, au kudhalilishwa ki ngono na hata kisaikolojia. Lakini wengi pia
wanateseka kazini kwa maisha magumu bila kuheshimiwa na waajiri wao.
Sheria mpya zilizotangazwa na waziri wa kazi
nchini humo zinatarajiwa kusuluhisha hili.
Sheria zenyewe zinaamrisha waajiri kuwalipa
wafanyakazi wao mishahara yao kamili kwa muda walioagizana.
Waajiri pia wataskahiki kuwapa wafanyikazi wao
siku moja ya mapumziko katika wiki, na kutowafanyisha kazi zaidi ya saa tisa kwa
siku.
Sheria kwa waajiri
Walipe mishahara kamili kwa wakati unaofaa
watoe siku moja ya mapumziko kwa wiki kwa
wafanyikazi wao
wasiwafanyishe kazi zaidi ya saa tisa kwa
siku
Sheria hizo pia zinasema kuwa wafanyikazi
wanafaa kuwaheshimu waajiri wao na wasiache kazi bila sababu nzuri. Hata hivyo
changamoto kubwa ni kwa namna sheria hizi zitakavyotekelezwa.
Adhabu ya faini kali imewekwa kwa yeyote
atakayevunja sheria hizi.
Mamilioni ya wafanyikazi wa nyumbani hutafuta
ajira nchini Saudi Arabia wengi wao kutoka Ufilipino, Malaysia, Indonesia na
hata mataifa ya Afrika.
Baadhi ya mataifa yamesitisha vibali kwa raia
wao kusafiri nchini Saudi Arabia kufanya kazi za nyumbani kutokana na visa
vilivyokithiri vya unyanyasaji.
Sheria kwa Wafanyakazi
Lazima waheshimu waajiri wao
Lazima waheshimu dini ya kiislamu
Wasiache kazi au kukataa maagizo bila sababu
mwafaka
Post a Comment