MUSIC Computing ni
kampuni inayocheza na teknolojia, mbali na kutoa kompyuta yenye kasi ya
ajabu na disk yenye ukubwa wa 21 TB, kampuni hii pia ina gajeti nyingine
yenye kufurahisha, nayo ni Motion Command CT.
Kwa jina unaweza ukadhani
labda ni simulation ya ndege, kiuhakika hii ni meza ya kuweka ukumbini
(sebuleni).
Meza hii haiathiriki kwa maji (water proof) na ina skrini ya
kompyuta, skrini hii inakuja na kompyuta ya Android.
Pia inaweza
kufanya kazi na OS za Windows 7 na 8 pamoja na Mac OSX. Pia inakuja na
kompyuta ya Android.
Kwa mujibu wa Music
Computing watengenezaji wa meza hii, Motion Command CT ina skrini mguso
(touch screen), hivyo unaweza ama kutumia Android moja kwa moja au
kuiunganisha na tablet au laptop ya windows, na kwa upande wa Mac,
kompyuta ya rahisi zaidi kuiunganisha itakuwa ni Mac Mini.
Motion
Command CT inaweza kuunganishwa na kompyuta mbili sambamba. Ingawa
hazitafanya kazi kwa pamoja. Music Comptuing hawakueleza ni toleo gani
la Android lililopo kwenye kompyuta yameza hii.
Motion Command CT ina
USB, Wifi (kama utaamua kutumia Android tu), na HDMI, kwa apps ambazo
zimetengenezwa tayari kutumika na multi touch meza hii inakubali miguso
mingi sambamba kwa wakati mmoja (multi touch) Rezolushani za Motion
Command CT ni za HD kamili yaani 1920 x1080 (1080p). Pia inakuja na
rimoti kwa ajili ya kuwasha na kuzima tu.
Wakati skrini ina ukubwa
wa 32” meza yenyewe ina ukubwa wa 46.5” na unaweza kuchagua rangi
nyeusi au ya kahawia. Pia unaweza kuchagua skrini ndogo yaani yenye
ukubwa wa 22”, na idadi ya juu kabisa ya miguso sambamba inayokubalika
katika skrini hii ni 40.
Kwa vile inahimili maji basi unaweza pia
kunywea kahawa, au kinywaji chochote bila ya kuhofia kuiharibu.
Music Computing
wanaeleza kuwa meza ya Motion Command CT imetengenezwa kwa umadhubuti
maalum ambao unaruhusu meza hiyo kudumu kwa miaka kadhaa. Ili kuimiliki
meza hii unatakiwa kuunguza jumla ya $ 3,300 sawa na Shilingi za
Kitanzania Milioni 3.34, ongeza na gharama za usafirishaji kutoka
Marekani.
Post a Comment