Na Mahad Ibrahim,
Mogadishu
Kikundi cha wataalamu cha al-Shabaab cha tawi
la Amniyat kinaweza kuwa kikosi cha mwisho kinachomuweka madarakani kiongozi wa
kikundi cha wanamgambo Ahmed Abdi Godane kwa vile kikundi kinaendelea kupoteza
maeneo na makamanda wapinzani wanashinikiza uasi wao dhidi ya utawala wake,
waangalizi wasema.
Picha iliyotumwa
na al-Shabaab katika akaunti ya Twitter tarehe 29 Aprili, ikiaminiwa kuonesha
majeshi waaminifu kwa Godane. [Jalada]
Wanachama wa Amniyat wamepata mafunzo na
operesheni maalumu za hali ya juu ambao kazi zao zinajumuisha kukusanya habari
za kiintelijensia ili kutekeleza misheni za mauaji na kulipua mabomu.
Muundo wa uongozi wa Al-Shabaab umegawika
katika sehemu tatu: Jabhad, tawi la kijeshi; Hizb, ni sawa na polisi; na
Amniyat, kitengo cha kiintelijensia, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Redio Mogadishu
na aliyekuwa msemaji wa Mahakama za Kiislamu Abdirahim Isse Addow.
Askari wapya mwanzoni hupewa mafunzo makambini,
ambapo baadaye wakufunzi huwapeleka katika moja ya matawi hayo, alisema.
Amniyati pia huajiri watendaji kutoka matawi mengine ndani ya al-Shabaab.
"Mtu ambaye ni mbunifu, shujaa, mwaminifu kwa
emir [Godane] na itikadi za kikundi, na anayeweza kutunza siri huchaguliwa kuwa
mwanachama wa Amniyat," Addow aliiambia Sabahi. "Baadaye hupewa mafunzo maalumu
na hutengwa katika vitendo tofauti kama vile kikosi cha ulipuaji mabomu na
mabomu ya kuzika ardhini, kitengo cha milipuko, kitengo cha mauaji, na kitengo
cha intelijensia.
Hata hivyo, Amniyat kimekuwa kikidhoofishwa na
habari zinazotolewa na waasi na wapiganaji waliokamatwa, Addow alisema. Kwa
mfano, maafisa wa usalama huko Puntland walimjeruhi na kumkamata kamanda wa
Amniyat mwezi wa Juni.
Kwa vile operesheni nyingi kwa sasa zinalenga
katika kumaliza vitisho vya ndani dhidi ya utawala wa Godane, ikiwa Amniyat
kitashindwa na kumalizwa, hiyo inaweza kusababisha kumalizika kwa
al-Shabaab,
"Majeshi ya Jabhad yameshindwa na Hizb
hakifanyi kazi au kuudhibiti mkoa wowote," Addow. "Kwa hivyo, kitu pakee
kilichobakia kwa al-Shabaab sasa ni Amniyat, na ni lazima kutafuta hatua
nyengine za kiintelijensia ili kupambana nao kwa sababu kitu pakee ambacho
kinaweza kutumiwa dhidi ya intelijensia ni intelijensia. Mtu mwenye silaha
hawezi kumshinda mtu ambaye amejifunika."
Mbunge wa zamani wa Somalia Mohamud Abdullahi
Weheliye Waqaa alisema kuwa serikali lazima iimarishe uwezo wake wa kukusanya na
kuchambua intelijensia ili kutambua mahusiano baina ya wanachama wanaofanya kazi
wa Amniyat na Godane.
Vikosi vya serikali vinapaswa kufikiria kuazima
baadhi ya mbinu za al-Shabaab, kama vile kujiipenyeza na kuvaa kiraia katika
operesheni, alisema. "Nadhani ingekuwa vizuri ikiwa serikali ingeunda kitengo
kilichofunzwa [kujificha] ili kutekeleza operesheni ndani ya al-Shaabab," Waqaa
aliiambia Sabahi.
Waqaa, ambaye alitumikia bunge la mpito hadi
mwaka 2012, alipokea vitisho vya kuuawa wakati akiwa anafanya kazi kutokana na
msimamo wake mkali dhidi ya al-Shabaab.
Mwaka 2011, viongozi wa al-Shabaab kama vile
Mukhtar Robow Ali na Omar Hammami, maarufu kama Abu Mansour al-Amriki, walimuita
Waqaa kuwa ni "mshirika wa maadui wa Uislamu" na ikaripotiwa alitoa wito akatwe
kichwa. Mwaka 2012, Ali alitoa zawadi ya dola 100,000 ili auliwe, kwa mujibu wa
vyombo vya habari vya ndani.
Waqaa alisema kuwa mkabala mpya mpana
unahitajika ili kuwavunja al-Shabaab, ikiwemo kuwatumia ipasavyo wapiganaji wa
Amniyat ambao wamekamatwa kama vishawishi ili kufichua habari na kuboresha mbinu
za al-Shaabab.
Watendaji wa Amniyat wanapendelewa na
Godane
Watendaji wa Amniyat hupokea amri kutoka kwa
Godane tu, alisema Sheikh Mohamed Farah Ali al-Ansari, mkuu wa vituo vya
marekebisho vya serikali ya Somalia.
"Amniyat ndio wenye dhamana ya mauaji na
wanafanya kazi kwa siri," aliiambia Sabahi. "Wamepewa kazi ya kumuua yeyote
anayepingana na itikadi ya kikundi chao -- iwe ndani ya kikundi au nje yake.
Hakuna suala lolote juu ya mtu yoyote wanayemuua."
Wanachama wa kikundi hiki cha kitaalamu huwa
wanapokea motisha za ziada ambazo hazitolewi kwa matawi mengine ya kikundi, kwa
mujibu wa al-Ansari.
"Amniyat inapata mgao mkubwa zaidi wa bajeti
inayotengwa kwa ajili ya majeshi ya al-Shabaab," alisema. "Hawa hupewa simu za
mikononi zikiwa na pesa, wake na pesa taslimu kama njia ya kuwatia moyo."
Ingawa Godane anajulikana kama kamanda wa
Amniyat, hakuna safu ya viongozi wa kati wanaojulikana kwa sababu Godane
huwabadlisha mara kwa mara, al-Ansari alisema.
Kwa kuongezea, wageni nadra huruhisiwa
kushiriki katika misheni za Amniyat kwa sababu watendaji wa huko wanatakiwa wawe
wamejichanganyisha na umma wa Somalia.
"Wapiganaji [wa kigeni] huendesha mafunzo kwa
ajili ya Amniyat [kwa vile] wengi wao ni watu waliopewa mafunzo binafsi ambao
ujuzi wao unathaminiwa," alisema na kuongeza kwamba wapiganao wa kigeni hujiunga
na tawi la Jabhad wakati wa vita.
Wanachama wa Amniyat wanaojificha wameenea
katika mikoa tofauti na wanafanya kazi kwa siri, alisema al-Ansari, na kufanya
iwe vigumu kuwafuatilia na kuwamaliza.
"Hakuna kikundi kinachojua kuhusu wengine, kwa
mfano, vikundi vinavyofanya kazi Benadir na Baidoa havielewi chochote kimoja
kuhusu chengine. Huwa wanapokea mafunzo ya kijeshi, baadaye kila kitengo hupata
mafunzo yake ya siri [katika misheni moja moja]," al-Ansari alisema.
Chanzo - sabahionline.com
Post a Comment