Kundi la Al-Qaeda nchini Syria leo limemuuwa kiongozi wa waasi wa jeshi
huru la Syria FSA, Kamal Hamami na wapiganaji wengine wawili, katika
mapigano yaliojiri katika wilaya ya pwani ya Latakia nchini Syria.
Mapigano hayo yamezusha wasiwasi kati ya jeshi huru la Syria , wafuasi
wake na makundi ambayo yana mafungamno na mtandao wa Al-Qaeda ambayo kwa
kiasi kikubwa unawahusisha wapiganaji wasiokuwa wasyria.
Waangalizi wa haki za binadamu nchini Syria wamsema kuwa Kamanda Kamal
Hamami anayefahamika kwa jina maarufu la Abu Bassir al-Jeblawi, alipigwa
risasi na kundi linalopigania taifa la kiislamu nchini Iraq na Syria
ISIS, moja ya makundi yanayopigana vita vya jihadi nchini humo
Kamanda huyo wa waasi alipigwa risasi wakati wapiganaji wa kundi hilo la
ISIS wakijaribu kuharibu kituo cha ukaguzi cha jeshi huru la Syria FSA
katika mkoa wa Jabal al-Turkman kasikazini mwa wilaya ya Latakia
Kwa mujibu wa wachunguzi ambao wanategemea kwa upana taarifa kutoka
mtandao wa wanaharakati, madaktari na wanasheria, wamesema waasi wa
Jeshi Huru la Syria FSA walipiga risasi hewani na baada ya hapo
wapiganaji wa kundi la ISIS wakajibu mashambulizi yalimuuwa Abu Bassir
na kujeruhi wengie wawili wa kundi lake.
Jana kundi hilo la Kiislamu lilimuachia kiongozi mwengine wa waasi baada
ya kumshikilia kwa siku 25 sambamba na waasi wengine tisa. Juma
lillilopita wapiganaji kadhaa wa FSA waliuawa katika mapigano dhidi ya
kundi la ISIS katika jimbo la Idlib Kaskazini Magharibi
Hata hivyo wapiganaji wa kundi la ISIS wanatuhumiwa kwa kuwawake
kizuizini mateka kadhaa katika mji wa Raqa, mji mkuu pekee wa jimbo hilo
ambao upo nje ya udhibiti wa utawala wa Rais Bashar al-Assad.
Wanaharakati wanaompinga Rais Assad wanaoishi katika maeneo ya waasi
hivi sasa wanabadili mitazamo yao kwa kufanya kampeni dhidi ya
wapiganaji wa kundi la kiislamu lenye mafungamano na Al Qaeda kutokana
na ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu unaofanywa na kundi hilo.
Kwa sasa kuna makundi mawili nchini Syria yenye mafungamano Al-Qaeda
yote yakiwa na asili ya Iraq, kundi la Al-Nusra ambalo linajitegemea
katika harakati zake zake na ISIS .
Wakati huo huo Upinzani nchini Syria umeilaumu kamati ya Bunge la
Marekani kwa kupinga mpango wa kuwapa silaha waasi nchini syria,
ikihofia kwamba huenada silaha hizo zikaangukia mikononi mwa makundi ya
kiislamu ya siasa kali.Mnamo siku ya Alhamisi upinzani nchini Syria
ulitoa wito mwengine wa kupatiwa silaha, ukiahidi kwamba silaha hizo
hazitaingia mikononi mwa makundi ya Kiislamu.



Post a Comment