Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

UN:WAMEUAWA KATIKA MAPIGANO YA KIKABILA KENYA


UN: 181 wameuawa katika mapigano ya kikabila Kenya  
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, watu wasiopungua 181 waliuawa, 217 kujeruhiwa na wengine 52 elfu kuwa wakimbizi, kwenye mapigano ya kikabila yaliyotokea nchini Kenya.
Ofisi ya kuratibu misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA imeeleza kuwa, takwimu za mauaji, majeruhi na wakimbizi hao ni za  kutokea mwezi Januari mwaka huu hadi sasa. Msemaji wa OCHA katika Ukanda wa Afrika Mashariki Matthew Conway amesema kuwa, serikali ya Kenya kwa kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu la nchi hiyo, asasi zisizo za kiserikali pamoja na mashirika mengine ya kimataifa yametoa misaada ya kibinadamu kwa wakimbizi na majeruhi wa mapigano hayo ya kikabila. Conway ameongeza kuwa, mikoa ya Rift Valley, Magharibi na Kaskazini Mashariki mwa Kenya ndio iliyoathirika sana na mapigano hayo ya kikabila.
Taarifa ya OCHA imeeleza kuwa, wahanga wengi wa mapigano hayo ni kutoka maeneo ya kaskazini mwa Kenya, ambayo yalikubwa na mapigano makubwa kati ya makabila ya Garre na Degodia na kusababisha mauaji ya watu wasiopungua 70.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top