JESHI la wananchi JWTZ limesema kuwa linasubiri kibali kutoka kwa umoja
wa mataifa ili kujibu mapigo kwa waasi waliofanya shambulizi dhidi ya
kikosi cha UN na kuua wanajeshi saba watanzania huku wakiwajeruhi
wengine kadhaa.
Kanali Kapambale Mgawe alisema endapo wakipewa ruhusu kutoka kwa UN
watafanya hivyo lakini kwa sasa hawawezi kutokana na sheria zilizopo.
Aidha kanali mgawe ameongeza na kusema miili ya wanajeshi hao saba hivi
sasa inafanyiwa uchunguzi na timu ya wataalamu ya umoja wa mataifa na
kisha baada ya hapo italetwa nchini ambapo itahifadhiwa katika hospitali
ya lugalo na kisha baadae kupelekwa wizara ya ulinzi kwa ajili ya
heshima za mwisho kwa ndugu, jamaa na marafiki.
Ili kubaini chanzo cha kuuwawa kwa askari hao, tayari jeshi la wananchi
limeteua timu ya wataalamu ambayo itaelekea Darfur kuchunguza kwa kina
mauaji hayo ambayo ni makubwa kutokea kwa askari wanaolinda amani wa
umoja wa mataifa.
Umoja wa Mataifa waaswa:
Umoja wa mataifa umetakiwa kuangalia usalama wa wanajeshi wanaolinda
amani katika sehemu mbalimbali duniani ili kuzuia wanajeshi hao
kuendelea kushambuliwa na hatimaye kuuwawa pindi wanapokuwa kazini.
Kauli hiyo imetolewa na mhadhiri mwandamizi wa sayansi ya siasa na
utawala kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dr Lupa Ramadhani wakati
akielezea tukio la kuuwawa wanajeshi saba watanzania mjini Darfur nchini
Sudan.
Dr Lupa ameutaka umoja wa mataifa kutunga sheria zitakazozidi kuwalinda
wanajeshi wanaolinda amani ikiwezekana kulegeza sheria za sasa
zinazowazuia wanajeshi kupambana na waasi.
Kuhusianan na mahusiano ya kidiplomasia kati ya tanzaia na sudan kusini,
Dr Lupa amesema shambulizi hilo haliwezi kuathiri urafiki uliopo baina
ya nchi hizo kwani hata waasi hao hawatambuliwi na serikali ya sudan
kusini.
Post a Comment