Picha ya mzee
lifiga
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inasikitika
kutangaza kifo cha aliyekuwa mtabiri bingwa wa kwanza wa hali ya hewa na mkurugenzi mkuu wa kwanza wa Mamlaka ya Hali
ya Hewa Tanzania Bw. Urban Blass Lifiga. Bwana Lifiga alizaliwa tarehe 27
Novemba 1936, kifo chake kilichotokea Jumatatu tarehe 15 Julai 2013 mchana
katika hospitali ya Bosph Mbezi kwa Msuguli Dar es Salaam.
Bwana Lifiga alikuwa mtabiri bingwa wa kwanza Tanzania na
Mwaafrika wa kwanza kujiunga Idara ya Hali ya Hewa ya Afrika Mashariki iliyokuwa
chini ya Jumuia ya Afrika Mashariki, ambayo kwa wakati huu makao yake makuu
yalikuwa Nairobi, Kenya. Bwana Lifaga aliteuli kuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa
iliyokuwa Idara Kuu ya Hali ya Hewa, Tanzania. Alishisiriki na kushauri Serikali
katika kuanzisha kwa Idara hiyo.
Pamoja na nafasi ya Mkurugenzi Mkuu pia alichaguliwa kuwa
Mjumbe wa kudumu wa Tanzania katika Kamati Kuu ya Shirika la Hali ya Hewa Dunia.
Nafasi nyingine aliyeishika wakati wa uhai wake ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Hali ya Hewa ya Afrika Mashiriki.
Bwana Lifiga atakubumbuka kwa mchango wake mkubwa katika
kuendeleza sayansi ya hali ya hewa nchini, Afrika na Duniani.
Ni mmoja kati ya wanasayansi waliokuwa zao la chuo kikuu
cha Makerere na alichukua shahada ya udhamili chuo kikuu cha Nairobi. Hapa
nchini alipata mafuzo ya Sekondari katika shule za Kwiro Sekondari, Mahenge na
Pugu Sekondari, Dar es salaam.
Mazishi yanatarajiwa kufanyika Ijumaa tarehe 19 Julai 2013
nyumbani kwake Msakuzi.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inajumuika na familia,
ndugu, jamaa na marafiki katika kuomboleza msiba huu.
Bwana ametoa, bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe;
AMEN.
IMETOLEWA NA OFISI YA UHISIANO MAMLAKA YA HALI YA HEWA
TANZANIA
Post a Comment