MAKAMU
wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
Kongamano la Uwekezaji katika mkoa wa Tabora litakalofanyika keshokutwa
(Ijumaa) kwenye hoteli ya Serena jijini Dares Salaam.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dares Salaam na Mkuu wa Wilaya wa Tabora
Mjini Suleiman Kumchaya kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Tabora Fatuma Mwasa
wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano hilo.
“Tunamkaribisha
mtu yeyote aje kuwekeza Tabora kwa kuwa soko tayari lipo. Tunataka
kupandisha hadhi ya mkoa wa Tabora ili hali ya umasikini iondoke,”
alisema Kumchaya.
Akizungumzia
kuhusu hali ya mkoa huo, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora,
Longino Kazimoto alisema ni mkubwa kuliko miko mingine hivyo wanataka
uwe na maendeleo makubwa ndio maana wanawakaribisha wawekezaji kutoka
ndani na nje ya nchi.
Kazimoto aliongeza
kuwa mkoa huo una rasilimali za kutosha , ambazo ni misitu hekari
75,685 sawa na asilimia 44, ambapo asali inapatikana kwa wingi, mifugo
ipatayo milioni 3.2, matunda, hivyo wawekezaji wanaweza kuanzisha
viwanda vya kusindika.
Aidha
alisema mkoa huo hivi sasa kwa mwaka unaingizia Serikali Pato la
Taifa Sh. bilioni 1.2 na pato la mwananchi wa kawaida ni Sh. 560,783
kwa mwaka.
Kazimoto
alisema katika mkoa huo kuna vikundi 46 vya vijana ambavyo
vimeandaliwa ili kuweza kufuga nyuki kwa kisasa ili kuweza kupata asali
ya kusafirisha nje ya nchi.
Post a Comment