Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akifafanua jambo wakati
wa hafla ya uwekaji saini mkataba wa makubaliano kuhusu uzalishaji umeme
kwa mradi wa Kinyerezi III wenye uwezo wa kuzalisha umeme mega wati 600
kwa kutumia gesi asilia.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco
Mhandisi Felchesmi Mramba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Mhandisi Felchesmi Mramba kiweka saini mkataba wa makubaliano kuhusu
uzalishaji umeme kwa mradi wa Kinyerezi III wenye uwezo wa kuzalisha
umeme mega wati 600 kwa kutumia gesi asilia, waliosimama kutoka kushoto
ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Balozi wa China hapa nchini Balozi Lu Youging na Rais wa Kampuni ya China Power Investment, Lu Qizhou.
Profesa Muhongo alisema kuwa makubaliano hayo ambayo yanafanyika na Shirika la Umeme Nchi (Tanesco) na kampuni hiyo ya CPI utaweza kugharimu kiasi cha Dola milioni 300 hadi kukamilika.
Mkurugenzi wa Tanesco, Felchesmi Mramba akibadilishana hati na Mwenyekiti wa Kampuni ya Uwekezaji ya CPI, Lu Quizhou baada ya kuingia mkataba wa uwekezaji wa nishati ya Umeme kutoka China.
***********
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ameendelea kusisitiza na
kuwataka wakazi wa mkoa wa Mtwara kuelewa kuwa Gesi iliyopatikana katika
mkoa huo ni kwa ajili ya Watanzania wote.
Akizungumza
wakati akiwekeana makubaliano na kampuni ya uwekezaji wa nishati ya
umeme kutoka China (CPI), Profesa Muhongo alisema kuwa hata kama wakazi
wa mkoa huo watashindwa kuridhia uwekezaji wa nishati hiyo lakini gesi
hiyo ni kwa maendeleo ya Watanzania wote.
Profesa
Muhongo alisema kuwa makundi yanayopinga matumizi ya gesi hiyo
yanapaswa kuweka hadharani mikakati yao kuliko wanavyofanya sasa kwa
kupinga pasipo kutoa mipango yao.
Alisema
inapaswa kufika mahali Watanzania wakagawanywa katika makundi mawili
ikiwemo lile linalotaka maendeleo na linalopinga ili waweze kutengewa
maeneo.
“Hatuwezi
kuondoa umaskini kama tusipotumia gesi na raslimali tulizo nazo na hata
hili tatizo linalolalamikiwa sasa la vijana kukosa ajira litapata
ufumbuzi kama tutaweza kupanua uchumi wetu,” alisema.
Alisema kuwa Watanzania wanapaswa waache kulazimisha kufuata mawazo ya kupotosha.
“Tunataka
uchumi ukue, tuwe na umeme wa uhakika na hata bajeti yetu kuondoka
katika kuongeza bei katika bidhaa ndogo ndogo ili linaweza kufanikiwa
kama tukiwa na umeme wa uhakika na kutumia gesi yetu,” alisema.
Aidha
katika makubaliano hayo, Serikali imeingia makubaliano na kampuni hiyo
kwa kuzalisha umeme wa megawati 600 katika eneo la Kinyerezi namba 3
lililopo jijini Dar es Salaam.
Alisema
kuwa umeme huo utatumika kwa ajili ya matumizi ya kawaida na ifikapo
mwaka 2014 mwishoni wataweza kuuza megawati 500 kwa nchi za nje zenye
uhitaji wa nishati hiyo.
“Kupitia
uzalishaji huo tunategemea mwaka 2016 tutaweza kuzalisha megawati 1500
za nyongeza hatua hiyo itaweza kubadilisha uchumi wetu na kuwa na
bajeti yenye uhakika zaidi,” alisema.
Profesa Muhongo alisema kuwa makubaliano hayo ambayo yanafanyika na Shirika la Umeme Nchi (Tanesco) na kampuni hiyo ya CPI utaweza kugharimu kiasi cha Dola milioni 300 hadi kukamilika.
Post a Comment