|
[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
WILAYA YA MBARALI - AJALI YA PIKIPIKI KUGONGA GARI NA KUSABABISHA KIFO
MNAMO TAREHE
15/07/2013 MAJIRA YA SAA 16:15HRS HUKO MWAMBEGELE BARABARA YA MBEYA/IRINGA
WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. GARI NO .T605 AJP/T.693 AKE AIN YA SCANIA
LIKIENDESHWA NA DEREVA MOSHI S/O MZEE, MIAKA 42, MUHA, MKAZI WA IRINGA
LILIGONGWA NA PIKIPIKI ISIYOFAHAMIKA NA KUSABABISHA KIFO KWA ABIRIA WA PIKIPIKI
AITWAYE SIKUJUA D/O DAUDI, MIAKA
30, MSAFWA NA MKAZI WA MAJENJE IGURUSI.
MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI NA KUKABIDHIWA NDUGU
KWA MAZISHI. CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDO KASI WA PIKIPIKI NA KUSHINDWA
KUIMUDU KISHA KULIVAMIA GARI HILO KWA NYUMA. GARI LIPO KITUO CHA POLISI IGURUSI. DEREVA WA PIKIPIKI
ALIKIMBIA NA PIKIPIKI MARA BAADA YA AJALI HIYO JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA
MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI
ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE
TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO DEREVA ALIYESABABISHA AJALI AZITOE KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAKE ZICHUKULIWE, VINGINEVYO AJISALIMISHE
MARA MOJA.
WILAYA YA MOMBA -
AJALI YA MOTO NA KUSABABISHA KIFO.
NAMO
TAREHE 14/07/2013 MAJIRA YA SAA 06:00HRS HUKO KIJIJI CHA KAPELE KATA YA KATELE
WILAYAYA MOMBA MKOA MBEYA. MTOTO AITWAYW BRANDINA D/O ALINJITA, MIAKA 3, MNYAMWANGA ALIFARIKI DUNIA BAADA
YA KUUNGUA MOTO SEHEMU MBALIMBALI
ZA MWILI WAKE BAADA YA KIBANDA KILICHOJENGWA KWA NYASI KUUNGUA
MOTO WAKATI AKIWA NDANI NA WAZAZI WAKE WAKIWA SHAMBANI WAKIVUNA MAHARAGE.
CHANZO CHA MOTO HUO NI KIBERITI ALICHOKIWASHA MTOTO HUYO. TAARIFA KITUONI
TAREHE 15/07/2013 MAJIRA YA SAA 19:15 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA WAZAZI NA WAZEZI KUWA MAKINI
NA KUTOWAACHA WATOTO WADOGO NYUMBANI BILA UANGALIZI ILI KUWEZA KUEPUSHA MADHARA
YANAYOWEZA KUTOKEA.
WILAYA YA MBEYA - KUINGIA NCHINI BILA
KIBALI.
MNAMO
TAREHE 15/07/2013 MAJIRA YA SAA 09:0HRS HUKO UYOLE JIJINI MBEYA. ASKARI POLISI
WAKIWA DORIA/MISAKO WALIWAKAMATA
MALUKUSI S/O DEMSI, MIAKA 21, AKIWA NA WENZAKE SITA WOTE RAIA WA ETHIOPIA WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI [.]
WATUHUMIWA WAPO MAHABUSU TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA HUSIKA ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA
HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA ILI HATUA DHIDI YAO ZICHUKULIWE
HARAKA IKIWA NI PAMOJA NA RAIA WA KIGENI.
[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
|
on Tuesday, July 16, 2013
Post a Comment