Mshindi
wa Taji la Taifa la Miss Utalii Tanzania 2013, Hadija Saidi ambaye pia
ni Miss Utalii Morogoro 2012/13, sambamba na washindi wa Taifa na Dunia
wa Miss Utalii Tanzania, wataongoza warembo na washindi wa mashindano
yote ya urembo nchini na nchi jirani, katika mbio za nyika za kimataifa
za Ant Poaching International Marathon, National Parks International
Marathon na Wildlife International Marathon 2013, zitakazo fanyika
wakati wa Tamasha la kimataifa la Safari Kuu ya Utalii Tanzania la
“Tanzania Great Safari Tour ‘ 2013, litakalo fanyika kuanzia mwezi
Agosti hadi Septemba mwaka huu , katika Ukanda wa Kaskazini,
Kusini,Mashariki na Magharibi wa Utalii.
Mbio
hizo za kimataifa za Nyika za ANT POACHING MARATHON 2013, NATIONAL PARK
MARATHON 2013 na WILDLIFE MARATHON 2013 ni sehemu ya Tamasha la
kimataifa la SAFARI KUU YA KITALII TANZANIA 2013 yaani “TANZANIA GREAT
SAFARI TOUR 2013″ ambalo pamoja na malengo mengine linalenga katika
kuhamasisha vita dhidi ya Ujangili ikiwemo Uwindaji Haramu, Uvunaji
Haramu wa maliasili za Misitu na Baharini ikiwa ni pamoja na Uvuvi
haramu na Uharibifu wa Mazingira. Ujangili limekuwa ni janga la kitaifa
na tishio kubwa la Ustawi na ukuaji wa Utalii nchini na Duniani, ambapo
hatua na juhudi za pamoja zisipochukuliwa sasa basi wanyama waliopo
katika hifadhi za Taifa na Mapori ya akiba watatoweka na kuziacha
hifadhi hizo zikiwa hazina wanyama tena hasa Tembo,Vifaru,Twiga na jamii
nyingi za wanya ambazo hutumika kama kitoweo kwa binadamu.
Upo
ujangili wa uvunaji na usafirishaji haramu wa Misitu ambayo hutoa
magogo na mbao, na kuliacha Taifa likipoteza mapato ,huku uvunaji huo
haramu ukitishia maeneo ya misitu hiyo kuwa jangwa. Ujangili ukiachiwa
utakosesha watoto wetu na vizazi vijavyo Urithi wa Taifa, lakini pia
Taifa litapoteza Mapato yatokanayo na Utalii na Uvunaji mwingine wa
Maliasili za nchi. Ujangili ni uhujumu uchumi, kwani sekta ya Utalii
inachangia zaidi ya 17% ya Pato la Taifa kila mwaka, zaidi ya 25% ya
pato la fedha za kigeni la Taifa na zaidi ya 12% ya ajira zote nchini na
Duniani.
Tamasha
la “Tanzania Great Safari Tour 2013, nisafari kuu ya kitalii, ambayo
itawajumuisha na kuwaweka pamoja Waandishi wa Habari, Vyombo Vya Habari
vya TV,Redio,Magazeti, Majarida, Mitandao ya Internet, Mitandao ya
Kijamii na Tovuti. Warembo,Wanamitindo,Wanamichezo, Wana Muziki na
Wasanii wa Ngoma za Asili na Filamu, wakitembelea Hifadhi za Taifa
,Ngorongoro Crater, Mapori ya Akiba, Hifadhi za Bahari, Maeneo ya
Kitamaduni na Kihistoria huku wakipiga picha za vyombo vya habari vya
kitaifa na kimataifa vya Televisheni, Filamu,Video ,Minato, Matangazo
,Makala, Promo DVD’S ,Vipindi vya Televisheni na Majarida huku
wakihamasisha Utalii wa Ndani, Vita Dhidi ya Uwindaji Haramu, Uvuvi
Haramu, Ujangili na Uharibifu wa Mazingira, huku pia wakitangaza Vivutio
vya Utalii Vya Tanzania kitaifa na kimataifa.
Mbali
ya washiriki wa kitaifa , pia kutakuwa na washiriki wa kimataifa,
wanadiplomasia, Viongozi wa Serikali, Mashirika ya Kimataifa, Umma,
Binafsi na Washiriki binafsi ambao wataandikishwa au watakao hamasika
kushiriki. Tamasha la “Tanzania Great Safari Tour 2013 ni Tafsiri
vitendo ya Sera ya Taifa ya Utalii, Wanyama Pori, Misitu, Utamaduni
,Uvuvi na Mazingira. Hii itakuwa ni fulsa nyingine kwa Tanzania na
mamlaka zake za Utalii sio kutangaza Vivutio vya Utalii Tuu bali kupiga
vita Ujangili hususani uwindaji haramu kitaifa na kimataifa. Aidha hii
itakuwa ni fulsa kwa Makampuni, Mashirika, Asasi za Umma na binafsi
kujitangaza kupitia Tamasha hili kwani litarushwa moja kwa moja (LIVE)
katika Televisheni na Internet , na kuangaliwa na zaidi ya watazamaji
680 Milioni Duniani kote. Tamasha hili linaandaliwa na Africa Tourism
Promoshen Centre kwa kushirikiana na Miss Tourism Tanzania Organisation.
Post a Comment