RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete anatarajia kuzindua
ujenzi wa barabara na kufungua rasmi kivuko cha Ruvuvu mkoani Kagera.
Taarifa
ilio tolewa na Katibu mkuu wa wizara ya Ujenzi Balozi Herbert Mrango
kwa yvombo vya habari inasema kuwa Mheshimiwa Raisi Kikwete atazindua
kivuko hicho Julai 27 mwaka huu.
Kivuko
hicho chenye uwezo wa kubeba tani 35 ikiwemo magari madogo 4 na abiria
80 kwa pamoja, kinatoa huduma ya kuvusha magari na abiria katika mto
Ruvuvu eneo la Rusumo
Alisema
kabla ya ufunguzi wa kivuko hicho, Rais Kikwete ataweka jiwe la msingi
kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Kigoma-Biharamulo-Lusahunga yenye
urfu wa kilometa 154, Julai 26 mwaka huu.
“Jumapili
tarehe 28 Julai Rais Kikwete ataweka jiwe la msingi katika barabara ya
Kyaka-Bugene-Kasumulo yenye urefu wa kilometa 59.1 tukio litakalofanyika
katika kijiji cha Omugakorongo” alisema Balozi Mrango.
Alifafanua
miradi yote mitatu inagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na kwamba kutekelezwa kwa miradi hiyo itasaidia sekta ya
usafirishaji na kukuza uchumi wa mkoa wa Kagera.
Aliongeza
kuwa barabara na kivuko hicho vitaimarisha huduma ya usafirishaji
katika mkoa huo na kuboresha biashara na usafiri kati ya mkoa huo na
mikoa mingine pamoja na nchi za Burundi, Rwanda na Uganda
Post a Comment