Miili ya
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ waliouawa Darfur wiki iliyopita
Sajent Shaibu Shehe Othuman wa Mpendae na Koplo Mohamed Juma Ali wa Kwarara
imekabidhiwa leo kwa familia zao mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Zanzibar.
Marehemu hao wawili
wenye Asili ya Zanzibar ni miongoni mwa Askari saba wa JWTZ waliuawa walipokuwa
wakilinda amani chini ya Umoja wa Mataifa na Afrika UNAMID,huko Darfur.
Miili ya marehemu hao imewasili majira ya
saa 9 alasiri kwa ndege ya JW 90 34 aina ya Boing ikitokea katika Hospitali ya
JWTZ Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya kuwasili Uwanjani hapo
Miili ya Marehem hao ilipokelewa na Katibu mkuu Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais
Khalid Mohamed Salum akifuatana na Mwenyeji wake Bregedia Jeneral Kamanda wa
Bregedi ya Nyuki Sharif Sheikh Othuman Viongozi wa Vyama na Serikali,Wanafamilia
pamoja na Wananchi kwa ujumla.
Aidha huzuni ziliendelea kutanda kwa
ndugu na Jamaa waliofika kupokea maiti hizo za Wapiganaji wa Amani ya Dunia
chini ya mwenvuli wa UNAMID.
Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais Shughuli za Mazishi zitafanyika kesho saa nne za asubuhi
katika makaburi ya Mwanakwerekwe nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Aidha shughuli hiyo ya Mazishi
itaambatana na taratibu za kijeshi zitakazofanyika Makaburini
hapo.
Post a Comment