Juma lililopita limekuwa ni
la huzuni kwa wanabiafra na tasnia ya mchezo wa mbio za pole pole (jogging) mkoa
wa Dar es Salaam kwa ujumla. mwanzo mwa juma tulipokea taarifa ya msiba wa mke
wa katibu Mkuu wa Temeke Jogging (Rasmi) ndugu Togocho ambapo mazishi
yalifanyika maeneo ya kurasini Mivinjeni. Vilabu kadhaa vya jogging viliendelea
kuonesha umoja kwa kushiriki kwenye msiba huo na mingine.
|
Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya Biafra Henry Maseko (mwenye shati jeupe) akitoa nasaha kwenye msiba
wa mke wa ndugu Togocho |
Siku ya Jumatano wanachama
wa Biafra kundi la watoto Mtoro Elvis na kaka yake Jimmy Elvis (pichani chini)
nao walifiwa ni bibi yao mlezi ambapo mazishi yalifanyika huko Mlandizi mkoa wa
Pwani.
|
Jimmy
Elvis |
|
Mtoro akiwa na kocha
Willy |
Huzuni iliendelea
kutamalaki siku ya jumapili tarehe 7 Julai, 2013 ambapo alfajiri ya siku hiyo
klabu ya michezo ya Biafra ilimpoteza mwanachama wake mtoto Aboubakar Iddi
Maganga ambaye alifariki kwa ajali ya gari iliyotokea Kibaha mkoani Pwani.
Taarifa ziliwafikia Wanabiafra wakati wakiwa katika mazoezi asubuhi hiyo toka
kwa baba mzazi wa Aboubakar bwana iddi Maganga ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya
Utendaji ya Biafra. Mazishi ya marehemu Aboubakar yalifanyika katika makaburi ya
Kinondoni siku ya Jumatatu tarehe 8 Julai, 2013.
|
Kaburi alimozikwa Aboubakar
iddi Maganga |
|
Baadhi ya
waombolezaji |
|
Kaka nathan akiiwakilisha
Temeke Jogging |
|
Wafiwa; Iddi maganga na
mkewe |
|
Waombolezaji |
|
Rose Mwakibugi (mwenye
rasta) pamoja na Asia Mohamed (mwenyekiti wa kunduchi
kwanza) |
|
Mwenyekiti wa Kopa Original
Jogging Mustapha alikuwepo |
Tunamwomba Mwenyezi mungu
azilaze roho za marehemu wote mahala pema peponi.
credit: michuzi matukio blog
Post a Comment