Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Bw. Ntambi Bunyazu (kulia) akieleza kwa Vyombo vya Habari majukumu ya
Wizara hiyo baada ya ugatuaji wa usimamizi na uendeshaji wa shule za Sekondari,
katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari Jijini Dar es salaam ,
kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bi. Zamaradi
Kawawa.
Hayo yalisemwa na Afisa Habari wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ntambi Bunyazu, wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya majukumu ya wizara hiyo baada ya ugatuaji wa usimamizi na uendeshaji wa shule za sekondari jijini Dar es Salaama mwishoni mwa wiki.
Aidha, alifafanua kuwa jumla ya walimu 23,167 wa shule za msingi 17,682 na 5,485 wa sekondari, walishawasilisha madai yasiyo ya malimbikizo ya mishahara.
Hata hivyo, alisema hadi kufikia Juni 30, mwaka huu, jumla ya walimu 19,530 walikuwa wamelipwa Sh. bilioni 17.
Bunyazu alisema kati ya Julai hadi sasa, serikali imelipa madai ya malimbikizo ya mishahara ya walimu 31,779 yenye thamani ya Sh. bilioni 28.
CHANZO: NIPASHE
Post a Comment