Spika wa Bunge la Jamhuri ya Korea Kusini wiki iliyopita
alihitimisha ziara ya siku tatu hapa nchini aliyoianza tarehe 8 hadi 10 Julai
2013 ambapo alikutana na viongozi wakuu wa Taifa. Awali alikutana na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Spika wa Bunge la
Tanzania Mhe. Anne S. Makinda. Spika huyo pia akiambatana na Naibu Spika wa
Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai aliizuru Zanzibar na kukutana na Rais wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Mohammed Shein na Spika wa Baraza la
Wawakilishi Mhe. A.P. Kificho. Katika mazungumzo waliyofanya, jambo lililojikeza
na kupokelewa kwa mtizamo chanya ni lile la Tanzania kufungua Ubalozi nchini
Korea. Pichani Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne S. Makinda wa nne kushoto na
Spika wa Bunge la Korea Mhe. Kang Chang-Hee wa nne kulia wakiendesha mkutano
baina yao na wabunge wa nchi zote mbili ulifanyika jijini Dar es
Salaam.
Rais wa Zanzibar Dkt. Mohammed Shein
(kulia) akiwa na mazungumzo na Spika wa Bunge la Korea Kusini Mhe. Kang
Chang-Hee (kushoto). Katikati ni mkalimani.
Spika Kang akipokelewa na Spika wa Baraza
la Wawakilishi Mhe. A.P. Kificho mara tu baada ya kuwasili katika uwanja wa
ndege wa Zanzibar.
Picha ya pamoja ya viongozi hao baada ya
mkutano ambao baadhi ya mambo yaliyozungumziwa ni pamoja na Korea kuuwekeza hapa
nchini katika Nyanja ya TEHAMA.
Wajumbe wa mkutano kwa upande wa
Tanzania.
Spika wa Bunge la Korea Kusini Mhe. Kang
Chang-Hee akiushukuru ujumbe wa Tanzania kwa heshima kubwa mara baada ya
kumaliza ziara yake hapa nchini. (Na Prosper Minja – Bunge)
Rais wa Zanzibar Dkt. Mohammed Shein
akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job
Ndugai (Mb) wakati wa ziara ya Spika wa Korea visiwani Zanzibar.
Rais wa Zanzibar Dkt. Mohammed
Shein akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Job Ndugai (Mb) wakati wa ziara ya Spika wa Korea visiwani
Zanzibar
Post a Comment