Rais Jakaya Kikwete
--
Jumla
ya wahamiaji haramu 8509 kutoka nchi za Rwanda, Burundi na Uganda
wameondoka nchini kwa hiari yao baada ya agizo la Mh. Rais Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete lilitolewa hivi karibuni akiwa ziarani mkoani Kagera.
Wahamiaji hao haramu wametoka katika mikoa ya Kagera, Geita na Kigoma.
Kati
ya hao wahamiaji haramu 5521 wamerudi nchini Rwanda, 2744 wamerejea kwao
nchini Burundi na 244 warejea kwao nchini Uganda. Katika zoezi hilo
siraha zipatazo 60 zimerejeshwa kwa hiari zikiwemo siraha aina ya SMG na
Magobole.
Aidha,
zoezi hilo la kuwarejesha wahamiaji haramu limekwenda sanjari na
urejeshaji wa mali na mizigo ikiwemo jumla ya mifugo 1996 iliyorejeshwa
katika nchi za Rwanda, Burundi na Uganda.
Serikali
inapenda kusisisitiza kwamba imefurahishwa sana na ushirikiano
iliyouliopata kutoka nchi za Rwanda, Burundi na Uganda hasa katika
kuwapokea wahamiaji hao haramu na kushirikiana na Tanzania katika zoezi
hilo.
Aidha
, katika zoezi hilo idadi ya wahamiaji haramu waliondoka ni kwa hiari
na Serikali inawasihi wahamiaji haramu ambao bado wako nchini kuondoka
haraka iwezekanavyo kabla ya hatua ya kuwaondoa kwa nguvu hazijaanza.
Zoezi
la kurejea kwa wahamiaji haramu ni utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya
Kikwete, alipotoa siku 14 kwa wahamiaji kuondoka nchini kwa hiari ndani
ya kipindi hicho.
Imetolewa na
Idara ya Habari(MAELEZO)
Idara ya Habari(MAELEZO)
15 Agosti, 2013
Post a Comment