BARAZA Kuu
la Waislam Tanzania (BAKWATA) limeviomba vyombo vya dola kuendelea
kufanya uchunguzi kuhusu tukio la kuvamiwa,kupigwa na kujeruhiwa kwa
Imamu na waumini wa Kiislamu wakiwa msikitini wakati wa swala ya
Idd-el-Fitri iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Wilaya ya Kyela mkoani
Mbeya na kuhakikisha
Aidha baraza
hilo limesikitishwa na kitendo hicho, na kuvitaka vyombo hivyo
kuhakikisha kwamba wahalifu wote wanafikishwa mbele ya sheria.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa leo kwa kwa vyombo vya habari na Mufti wa Tanzania Sheikh
Issa Simba,imelaani kitendo hicho na kusema watu waliofanya kitendo
hicho wamegeuka maagizo ya ya Qur’an Tukufu pamoja na Sheria za Nchi.
“BAKWATA
imewataka wananchi wote kufuata taratibu sahihi jambo lolote linapo
tokea.”Kama yupo mtu yoyote ana manung’uniko au hoja yoyote dhidi ya
mwenzake au taasisi yoyote,ni lazima watumie taratibu sahihi za kidini
au za kisheria na sio kuchukua sheria mkononi”alisema Sheikh Issa.
Alisema baraza hilo linamuomba Mwenyezi Mungu awaponye watu wote waliathirika na tukio hilo.
Post a Comment