|
Mmoja
wa majambazi waliouawa jana kwenye kituo cha mafuta GBP Mwanza jana majira ya
saa 2 usiku. |
Tumezipata
taharifa hizi kutokwa kwa moja wa wafanyakazi wa kituo cha mafuta cha GBP Mwanza
ambapo majambazi hawa walijalibu kuvamia ili kuiba.Ndugu Mohamed Sleyim Naddabi
alisema,
"Jambazi hili lilikuwa
limeshika panga.Mwenzake aliyekuwa na SMG alipoanguka huyu akaelekea mbio
kuichukua lakini akapambana na risasi ya polisi naye akagalagala
chini."
|
Jambazi jingine lililouliwa jana likitaka kupora
sheli ya GBP Mwanza . |
Ndugu aliendelea
kusema."Hilo hapo pichani lilikuwa na SMG.Lilitoka
kwenye gari likapiga risasi juu na kuanza kuelekea alipo Mhudumu wa pampu.Kidogo
lilisita baada ya kuona kushoto kwake mita kama 15 hivi kuna mtu mwenye silaha
ambaye ni polisi aliyevaa kiraia.Lilipotaka kumlenga yule polisi alifyatua
risasi iliyolenga sahihi kabisa na kichwa chake!"
on Wednesday, August 14, 2013
Post a Comment