Chama cha Wananchi, CUF, Zanzibar nchini
Tanzania kimeelezea kushtushwa na tukio la kumwagiwa tindikali kwa raia wawili
wa Uingereza katika maeneo ya Mji Mkongwe Zanzibar.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na
Salim Biman, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Habari, Uenezi, Mawasiliano na Umma
imesema CUF inalaani kwa nguvu zote tukio hilo la kikatili la kuwamwagia tindi
wageni hao ,na kinawataka polisi Zanzibar kufanya uchunguzi wa kina na waharaka
pamoja na kuhakikisha kuwa wale wote waliohusika na tukio hilo la kikatili
wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Taarifa ya Chama cha CUF imesema kama
ninavyonukuu, “hii ni dalili mbaya kwa Zanzibar kwani matukio haya ya tindikali
yamekuwa yanaonekana kama ni masuala ya kawaida jambo ambalo linatishia uchumi
wa Visiwa vyetu.
Post a Comment